Halmashauri ya Wilaya ya Mtama
DUTIES AND RESPONSIBILITIES
- Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari;
- Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi;
- Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari;
- Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali;
- Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari;
- Kufanya usafi wa gari; na
- Kufanya kazi nyingine kadri atakavyoelekezwa na Msimamizi wake.
QUALIFICATION AND EXPERIENCE
Mwombaji awe mwenye elimu ya kidato cha Nne (Form IV) au Sita (Form VI) na Leseni ya Daraja C au E ya Uendeshaji Magari ambayo wamefanyia kazi kwa muda usiopungua wa mwaka mmoja (1) bila kusababisha ajali Pamoja na vyeti vya mafunzo vilivyowapatia sifa ya kupata madaraja husika. Wawe wamehudhuria mafunzo ya Misingi ya uendeshaji magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na Chuo cha VETA au Chuo kingine kinachotambulika na Serikali.
APPLICATION TIMELINE: 2025-07-09 2025-07-23
.