images (1)

AUA MTOTO KISA UGUMU WA MAISHA

WhatsApp
Twitter
Email
LinkedIn
Instagram

Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 19 aitwae Johari, Mkazi wa mtaa wa Kigamboni Mkoani Iringa amekamatwa na Polisi kwa tuhuma za kumtumbukiza kwenye ndoo ya maji ya lita ishirini na kumuua Mtoto wake mwenye umri wa miezi saba kutokana na kile alichodai kuwa ni maisha magumu.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Mawelewele Obedi Mtatifikolo amesema kuwa walipomuuliza Johari kwanini amefanya maamuzi hayo magumu alisema alikuwa akiishia kwenye mazingira magumu yaliyopelekea kukosa hata sabuni ya kumuogeshea Mtoto wake na kwamba hata Kaka yake alikua akimuambia hakustaili kuwa na huyo Mtoto.

Johari amechukuliwa na Polisi kutoka eneo la tukio ambalo ni Mawelewele kata ya Mwangata Manispaa ya Iringa ambako ndiko Mtuhumiwa anakodaiwa kumuua Mtoto wake kwa kumuingiza kwenye ndoo kichwa chini miguu juu.

WhatsApp
Twitter
Email
LinkedIn
Instagram

Related