download (3)

BANGI YETU HAIFAI HATA KWENYE MASOKO HALALI HUKO NJE

WhatsApp
Twitter
Email
LinkedIn
Instagram

Kamishna wa Kinga na Tiba kutoka Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Dkt. Peter Mfisi amesema Nchi zilizohalalisha bangi zina utaratibu thabiti ikiwemo kulima bangi hizo kwenye maeneo maalum na kuna kiwango kinachotakiwa ambapo amesema bangi ya Tanzania inayolimwa kwenye mashamba yasiyo rasmi kiholela haifai na haiwezi kukubalika kwenye masoko halali ya nje ya Nchi.

Amesema hayo leo Jijini Dar es salaam ”“Nchi zilizohalalisha bangi wana bangi yao inalimwa kwenye green house inatakiwa iwe na kiwango fulani, tusichukulie tu jambo la rahisi tu kwamba tutachukua tuweke kwenye kiroba kwenda kuwauzuia nje mfano Kenya, Kenya wenyewe bangi haijahalalishwa”

“Hii bangi yetu haifai kwenye kwenye masoko halali hata huko nje, kule wenzetu wametengeneza sehemu maalum za kuuza, kiwango cha kununua na hata umri wa Mtu wa kumuuzia, ukisema uruhusu ya kwetu haiwezi kukubalika, mfano halisi ni miwa, hivi miwa yote inaruhusiwa kutengenezea sukari?, jibu ni hapana, na bangi pia ipo hivyo sio kila bangi inafaa kwa matumizi halali”

WhatsApp
Twitter
Email
LinkedIn
Instagram

Related