Nafasi ya kazi :- NAHODHA DARAJA LA II (SKIPPER)

UTUMISHI_423.jpg

Halmashauri ya Wilaya ya Mafia

Positions
2 Positions

Application Period
31/07/2026 - 12/08/2026

Duties and Responsibilities
  • Kuendesha boti ya doria;
  • Kubuni, kutengeneza na kutunza zana za kuvulia samaki (Fishing Gears);
  • Kuongoza na kuendesha boti/meli ndogo zenye urefu wa futi 40 na uzito wa kuandikishwa wa tani 50 – 100 “Gross Tonnage (GRT)”;
  • Kuendesha shughuli za uvuvi katika meli; Kushiriki katika kuendesha doria za baharini na nchi kavu, na Doria za EEZ;
  • Kusoma taarifa za VMS na kuziwasilisha kwa Mkuu wa kituo kila siku, wiki, mwezi, robo mwaka, nusu mwaka na mwaka;
  • Kukamata wahalifu wa Sheria na Kanuni za Uvuvi;
  • Kusaidia kutunza Kumbukumbu zote za matumizi ya mafuta katika vyombo vya doria;
  • Kusaidia kuandaa ratiba ya kufanya matengenezo na “service” ya vyombo vyote vya doria (service schedule);
  • Kutekeleza majukumu yote ya kikosi kama yalivyoainishwa katika Kifungu cha 32 cha Sheria ya Uvuvi na. 22 ya mwaka 2003; na
  • Kufanya kazi nyingine za fani yake atakazopangiwa na mkuu wa kazi.

Qualifications
Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha IV au VI wenye Stashahada (Diploma NTA – level 6) ya Unahodha na Uvuvi (Master Fisherman) kutoka Vyuo vya Wakala wa Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (Fisheries Education and Training Agency – FETA) au sifa inayolingana na hiyo kutoka vyuo vingine vinavyotambuliwa na Serikali.

Remuneration