Crude-oil-eacop

MAOMBI YA KUONESHA NIA YA UTOAJI WA HUDUMA ZA USANIFU NA UTEKELEZAJI WA UREJESHAJI WA MAKAZI NAMAZALIO YA MATUMBAWE KWA AJILI YA VIUMBEHAI WABAHARINI NA MIPANGO YA UREJESHAJI WA MAZINGIRA KATIKA HALI BORA ZAIDI MKOANI TANGA: KUMBUKUMBU NA: REQ-00000197

WhatsApp
Twitter
Email
LinkedIn
Instagram

Kampuni ya Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) Ltd, L”EACOP LTD*)
inakaribisha kampuni zenye uzoefu na weledi wa kutosha kuonesha nia ya kutoa huduma ya
urejeshwaji wa Makazi na Mazalio ya Matumbawe kwa ajili ya viumbehai wa baharini na mipango
ya kurejesha mazingira katika hali bora zaidi mkoani Tanga katika Mradi wa EACOP.

Madi wa EACOP unajumuisha shughuli za ujenzi na undeshaji wa bomba la kusafirisha Mafuta
ghafi lililofukiwa chini ya ardhi linalokatisha mipaka ya nchi mbili (Tanzania na Uganda) kwa ajili
ya kusafirisha Mafuta ghafi kwenda masoko ya kimataifa. Bomba litaanzia Kabaale katika Wilaya
ya Hoima, nchini Uganda, mpaka rasi ya Chongoleani, Mkoani Tanga, nchini Tanzania. Urefu wa
bomba ni kilomita 1,443, kati yake kilomita 1,147 zitakuwa nchini Tanzania.

MAELEZO MAFUPI KUHUSU HUDUMA

Miundo mbinu ya EACOP katika rasi ya Chongoleani inajumuisha Kituo cha kuhifadhi Mafuta
(MST), magati mawili, Kituo cha Kupakua mafuta (LOF). Eneo dogo la Matumbawe kwa ajili ya
makazi na mazalio ya viumbehai wa baharini litaguswa na shughuli za ujenzi na vendeshaji wa
gati. Mpango kazi wa Bayoanuai (BAP) unaoeleza takwimu za awali za maeneo yaliyoguswa na
mradi umeandaliwa.

Kampuni/mshauri wa kitalaamu au taasisi yenye weledi inahitajika kwa ajili ya kusanifu na
kutekeleza mango wa urejeshaji wa makazi na mazalio ya Matumbawe kwa ajili ya viumbehai wa
baharini na mipango ya kurejesha mazingira katika hali bora zaidi katika eneo la maji ya kina
kifupi kwa kuzingatia vigezo na mbinu bora, kujifunza kutokana na mipango iliyopo katika eneo
hilo, na kwingineko katika ukanda huu au duniani kote. Mbinu inayopendekezwa ni pamoja na
urejeshaji wa ekolojia ya matumbawe kijamii (CBECR) unaohusisha wadau wa ndani na makundi
engine kutoka eneo hilo ikiwa ni pamoja na jamii za wenyeji, taasisi za serikali na Mashirika ya
kiraia. Maamuzi ya urejeshaji yatapaswa kuzingatia data za kisayansi ili kuweka mizania sawa
kulingana na hali iliyopo ya kijamii na kimazingara na mabadiliko tarajiwa ya baadaye.

VIGEZO MUHIMU:
Makampuni a taasisi zinzoonesha nia zinakaribishwa kutuma maombi na kuambatanisha
nyaraka zifuatazo.

  • Uthibitisho wa usajili wa taasisi ambayo shughuli zake zinahusisha ushirikishwaji wa jamii (kama vile ushiriki wa jamii katika urejeshaji wa makazi katika Matumbawe kwa ajili ya viumbehai wa baharini) nchini Tanzania.
  • Taarifa fupi kuhusu uzoefu na uwezo wa kusanifu na kutekeleza mango wa urejeshwaji wa makazi na mazalio ya Matumbawe, kwa kufanya kazi na kujenga uwezo wa jamii ya watu wa pwani, kuanzisha vitalu vya matumbawe, kufanya utafiti jaribizi kuhusu matumbawe, kufuatilia na kutathimini hali ya matumbawe a kubaini maneneo yanayofaa kwa urejeshaji wa makazi katika matumbawe kulingana na sifa za kimaumbile, kihaidrolojia na kibayolojia.
  • Mifano ya shughuli zinazoonyesha uzoefu wa kufanya shughuli ya urejeshaji kama hii, ambazo taasisi imetekeleza kwa kipindi cha hivi karibuni: ndani ya miaka mitano
  • Wasifu wa wafanyakazi muhimu watakaohusika katika mradi ikiwa ni pamoja na yeti vya lazima vya wahudumu na viwango vya elimu, pamoja na uzoefu na uwezo wa kutoa huduma zinazotakiwa.
  • Leseni halali, kama ipo, kutoka mamlaka ya ndani ya chi husika kwa ajili ya utoaji wa huduma husika.
  • Uthibitisho wa kusajiliwa a Mamlakaya Mapato Tanzania (TRA) na Cheti cha Mlipa kodi cha mwaka wa hivi karibuni.
  • Waombaji wanasisitizwa sana kuhakikisha kuwa wamejisajili kwenye kazidata ya EWURA (LSSP) ya Watoa Huduma za Ugavi wa Ndani. wakati wa kuwasilisha maombi ya kuonesha nia,
  • Kukidhi vigezo na Kanuni za watoa huduma Wazawa za mwaka 2017.
  • Uwezo wa kifedha wa kutoa huduma zinazohitajika ikiwa ni pamoja na kuwasilisha hesabu za fedha za miaka mitatu iliyopita
  • Uthibitisho kutoka kwenye mfumo wa Usimamizi wa QHSE, taasisi na mchakato kulingana na Viwango vya Ndani na vya Ki-Sekta vinavyotumika kwa kazi kama hii.
  • Uthibitisho wa sera ya kupinga vita rushwa, ufisadi, na kuzingatia Haki za Binandamu.

Kampuni zenye nia, uwezo na rasilimali za kutosha kutekeleza shughuli zilizota¡wa hapo juu
zinakaribishwa kutuma maombi pamoja na kuambatanisha nyaraka zilizotajwa hapo juu kupitia
barua pepe ya [email protected] , (ukubwa wa barua pepe usizidi 20Mb). Maombi
yatumwe kabla au mnamo tarehe 12 May 2023, saa 11 jioni saa za Afrika Mashariki. Kichwa cha
Barua pepe kiwe 00000197 – Utoaji wa huduma ya urejeshwaji wa Makazi katika Matumbawe kwa
ajili ya viumbehai na mipango ya kurejesha mazingira katika hali bora zaidi mkoani Tanga katika Mradi wa EACOP Maombi yote ya kuonesha nia yawe kati ya kurasa 10 hadi 20 Maombi yote
lazima yaandikwe kwa lugha ya Kingereza

Muhimu: Kampuni ya EACOP LTD itapitia na kuchambua nyaraka zilizotumwa na makampuni
yenye nia kulingana na EOI hii na kisha kufanya tathmini kwa kutumia vigezo vya ndani ili
kubaini makampuni yatakayojumuishwa kwenye orodha ya (Makampuni) ya awali yaliyokidhi
vigezo. Makampuni yaliyofuzu hatua za awali pekee ndiyo yatakayopewa mwaliko wa zabuni, kwa
kutia saini Mkataba wa Kutunza Siri (NDA), kama mwendelezo wa wito wa mchakato wa utoaji
wa zabuni. Kampuni ya EACOP LTD inayo haki ya kufanya maamuzi yake ya kuchagua au
kukataa
kampuni na kubaki na maamuzi yake pasipo kutoa sababu kwa kampuni husika

WhatsApp
Twitter
Email
LinkedIn
Instagram

Related