JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
HALMASHAURI YA MANISPAA MOROGORO
TANGAZO LA ZABUNI
LGA/079/2020-2021/HQ/NCS/20
MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MANISPAA YA MOROGORO ANAWATANGAZIA WANANCHI WOTE KUTUMA MAOMBI YA KUPANGA VYUMBA VYA BIASHARA 187 KATIKA SOKO LA CHIFU KINGALU WANANCHI WOTE MNAKARIBISHWA.
FURSA ZA KIBIASHARA ZILIZOPO
Na | Aina ya fursa | Idadi | Bei ya fomu |
Vyumba vya biashara soko la chifu kingalu | 187 | 50,000.00 |
Malipo yote yatafanyika ofisi kuu Manispaa ya Morogoro mara tu baada mwombaji kupatiwa namba ya malipo (Control number), Fedha hizi hazitorejeshwa.
VIGEZO KWA MUOMBAJI
- Nakala halali ya leseni ya biashara .
- Nakala ya kitambulisho cha Taifa , cha mpiga kura au leseni ya udereva.
- Picha mbili za pasipoti.
- Barua ya utambulisho kutoka kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa anakoishi pamoja na namba za simu za Mwenyekiti.
- Mwombaji awe na Mdhamini mmoja( mtumishi wa umma).
- Nakala ya cheti cha mlipa kodi (TIN NUMBER)
- Mwombaji awe tayari kufungua biashara ndani ya wiki mbili baada kushinda zabuni hii.
Fomu za maombi zinapatikana katika ofisi ya Manunuzi (PMU) Manispaa ya Morogoro kuanzia Tarehe 20/05/2021saa 01:30 asubuhi hadi saa 09:30 alasiri, siku,ya jumatatu hadi ijumaa
Siku ya mwisho ya kuwasilisha fomu za maombi ni tarehe 02, Juni,2021 saa 6.00 mchana siku ya Jumatano, fomu zitafunguliwa hadharani mara baada ya kufunga zoezi la kupokea fomu hizo, ufunguzi utafanyika mbele ya wawakilishi watakao hudhuria katika ufunguaji wa fomu utakao fanyika 02, Juni,2021 saa 6.00 Mchana katika ofisi za Manispaa ya Morogoro Mashariti mengine, namba ya vioski na mahali vilipo vitaelezwa katika Fomu ya maombi.
NB: Waheshimiwa Madiwani, Watumishi wa Manispaa ya Morogoro,Watumishi wa Ofisi ya Mkuu mkoa na Mkuu wa wilaya hawaruhusiwi _kushiriki zabuni hii.
WANANCHI WOTE MNAKARIBISHWA.
Sheilla E. Lukuba
MKURUGENZI WA MANISPAA
MOROGORO