nmb

MWALIKO WA UCHAMBUZI WA AWALI WA
WAZABUNI WA VIFAA VYA STESHENARI

WhatsApp
Twitter
Email
LinkedIn
Instagram
  1. Benki ya NMB (“Benki”) ni benki ya biashara yenye mamlaka kamili iliyoorodheshwa katika
    Soko la Hisa la Dar es Salaam nchini Tanzania. Benki inatoa huduma za kibenki kwa watu binafsi, wafanyabiashara wadogo, wa kati, wateja wa makampuni makubwa na serikali. Benki hii ina mtandao mpana wa usambazaji huduma wa kielektroniki na kidijitali, unaowapa wateja wake chaguo la kupata huduma za kibenki.
  2. Benki imetenga fedha kwa mwaka 2023, kwa ajili ya gharama za uendeshaji wa mtandao wa
    matawi yake kote nchini. Inakusudiwa kuwa sehemu ya fedha hizi itatumika kwa malipo
    yanayostahiki chini ya mkataba kwa ajili ya utoaji wa huduma mbalimbali za Benki ikiwamo
    steshenari.
  3. Kwa sasa kamati ya zabuni ya Benki inawaalika wazabuni/wauzaji wa vifaa vya steshenari
    wenye vigezo, sifa na uzoefu kutuma maombi yao kwa ajili ya uchambuzi wa awali wa vigezo vya uzabuni.
  4. Uteuzi wa wazabuni wanaostahili na wenye sifa katika huduma husika utafanyika kwa taratibu
    za ushindani kama ilivyoainishwa katika sera na taratibu za manunuzi za Benki.
  5. Vigezo vya uteuzi vitajumuisha:
    • Kuhakiki cheti cha usajili wa kampuni kutoka kwa mamlaka husika, leseni ya biashara, nakala ya cheti cha usajili wa mlipa kodi (TIN )na nakala ya cheti cha kodi ya ongezeko la thamani kwa waliokidhi vigezo (VRN)
    • Kampuni au mtoa huduma lazima awe na uzoefu usiopungua mwaka mmoja katika Nyanja husika na uzoefu wa kufanya kazi na mashirika mbalimbali,
    • Eneo la sasa (vithibitisho vitakaguliwa); hii inajumuisha nyaraka halali ya umiliki wa ofisi au mkataba wa kukodisha. Tafadhali kumbuka kuwa katika kutathmini maombi, sifa, uzoefu juu ya kazi zinazoendana na hii na uwezo wa kutoa huduma vitazingatiwa. Kampuni zinazostahili, zilizo na sifa na uzoefu ulioonyeshwa na rekodi bora za utendaji wa kazi zinazofanana na hii tu ndizo zitazingatiwa.
  6. Waombaji lazima wajumuishe nyaraka moja halisi na nakala ya maombi yao ya uzabuni. Nyaraka lazima zijazwe na kufungwa vizuri katika bahasha. Juu ya bahasha kuandikwe “Uchambuzi wa Awali wa Wazabuni wa Vifaa vya Steshenari”. Maombi yaainishe tawi la Benki mzabuni aliloomba kulihudumia. Nyaraka hizo zifikishwe kwenye tawi la Benki lililo karibu au Ofisi ya Kanda ya Benki kwa anuani; Katibu Kamati ya Usimamizi wa Zabuni ya Benki ya NMB PIC, Mtaa wa Ohio/Barabara ya Ali Hassan Mwinyi, S.L.P. 9213, Dar es Salaam, Tanzania. Muda na tarehe ya mwisho ya kuwasilisha zabuni kwa maandishi ni Ijumaa tarehe 27 Machi 2023 saa tisa alasiri (“Tarehe ya Mwisho ya Kuwasilisha Zabuni”).
  7. Maombi yatakayochelewa, maombi yasiyokamilika, maombi ya kielektroniki na maombi
    ambayo hayakupokelewa kwa wakati kama ilivyoainishwa katika tarehe ya Mwisho ya
    Kuwasilisha Zabuni hapo juu, hayatazingatiwa katika tathmini bila kujali sababu ya kuchelewa
    ama kutokukamalika kwake.

Afisa Mtendaji Mkuu
P.O. Box 9213, Dar Es Salaam, Tanzania.
Benki ya NMB Plc. Makao Makuu Makutano ya Barabara za Ohio/Ali Hassan Mwinyi
www.nmbbank.co.tz

WhatsApp
Twitter
Email
LinkedIn
Instagram

Related