Crude-oil-eacop

MWITO WA KUWASILISHA OMBI LA ZABUNI YA HUDUMA ZA FORODHA. MAREJEO.: 1020-EOI-GAC EI-TZ GEN-HUDUMA ZA FORODHA

WhatsApp
Twitter
Email
LinkedIn
Instagram

Mkandarasi EITS (Electrical Instrumentation and Telecommunications Systems) wa mradi wa
EACOP, anakaribisha mashirika yenye uzoefu na sifa nzuri kuwasilisha nia katika utoaji huduma
tajwa hapa chini
AINA YA KAZI
 Kufanya ukaguzi na vibali na mamlaka zilizoteuliwa kwa niaba ya EITS
 Kushughulikia usafirishaji wa mizigo, uondoaji wa forodha, usafirishaji (pamoja na
usafirishaji wa mipakani).
 Kuwasilisha hoja za njia ya usafirishaji / EACOP kuhusiana na kutolewa kwa mizigo
inayoingia kwa njia ya bahari/anga.
 Mtoa Huduma anatakiwa kuzingatia viwango vya juu vinavyohitajika katika nyanja zote
 Kutekeleza majukumu mengine yanayohusiana na bali maalum na Mradi wa EACOP
VIGEZO VINAVYOHITAJIKA
 Awe ni Biashara yenye Leseni Kamili na Uthibitisho wa Usajili na Mamlaka husika za
Tanzania ikiwemo Mamlaka ya Mapato Tanzania.
 Awe na cheti cha mlipa kodi cha hivi karibuni.
 Usajili kwenye kanzidata ya wasambazaji na watoa huduma wa ndani (LSSP) wakati wa
kuwasilisha jibu la maombi haya (EOI) ni lazima.
 Kuzingatia kanuni za maudhui ya Ndani za 2017; Sheria ya Petroli ya 2015 na ufafanuzi wa
kampuni ya ndani kwa Tanzania.
 Awe na taarifa za fedha za miaka 3 Iliyopita
 Awe na vyeti vya uthibitisho vya ISO 9001, ISO14001, ISO 45001
Makampuni zenye nia ambazo zinakidhi vigezo na zina uwezo wa kutoa huduma zilizoorodheshwa
hapo juu, zinapaswa kueleza nia yao kwa kutuma barua pepe pamoja na hati zilizoorodheshwa
hapo juu kwa [email protected] (isiyozidi 20mbs). Na namba ya kumbukumbu hapo juu iwe
kama kichwa cha baruapepe.
Nyaraka zote lazima ziwasilishwe kwa lugha ya Kiingereza na nambari ya kumbukumbu ifikapo
Februari 28, 2023 5:00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.

MKANDARASI anahifadhi haki ya kutozingatia makampuni ambayo yanawasilisha ripoti
isiyokamilika! Kumbuka: Kampuni zilizokidhi vigezo ndizo zitapokea mwaliko wa kuwasilisha
zabuni zao kwa ajili ya hatua nyingine za mchakato wa Zabuni.

WhatsApp
Twitter
Email
LinkedIn
Instagram

Related