Halmashauri ya Wilaya ya Iringa
DUTIES AND RESPONSIBILITIES
i. Kuendesha mitambo kikamilifu bila kusimamiwa.
ii. Kuweka vipimo mbalimbali vinavyotakiwa kufuatana na kazi anayofanya na
jinsi anavyoelekezwa na kiongozi wa kazi hiyo.
iii. Kutoa huduma ya kwanza ya matengenezo ya mitambo na pia aweze kutoa
maelekezo sahihi ya ubovu wa mitambo anapotakiwa kufanya hivyo.
iv. Kuandika vizuri ‘log sheet’ na kuweka kumbukumbu sahihi ya matumizi ya
vifaa kwa mfano mafuta, grisi na vipuri.
v. Kuhakikisha kuwa mashine/mitambo inatumika kwa kazi zinazotakiwa.
vi. Kufanya usafi wa mtambo.
vii. Kufanya kazi nyingine kadri atakavyoelekezwa na Msimamizi wake
QUALIFICATION AND EXPERIENCE
Awe na cheti cha Mtihani wa Kidato cha Nne (IV), mwenye leseni daraja ‘G’ ya uendeshaji mitambo pamoja na ujuzi wa kutunza vyombo mbalimbali vya mitambo
hiyo, wenye uzoefu wa kuendesha mitambo kwa muda usiopungua saa mia tatu (300) au miezi mitatu (3) bila kusababisha ajali
APPLICATION TIMELINE: 2024-09-19 2024-09-28
.