Halmashauri ya wilaya ya Chalinze
DUTIES AND RESPONSIBILITIES
i. Afisa Masuuli na Mtendaji Mkuu wa Serikali ya kijiji,
ii. Kusimamia ulinzi na usalama wa raia na mali zao, kuwa mlinzi wa amani na msimamizi wa utawala bora katika kijiji,
iii. Kuratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya kijiji,
iv. Katibu wa mikutano na kamati zote za Halmashauri ya kijiji,
v. Kutafsiri na kusimamia sera, sheria na taratibu.
vi. Kuandaa taarifa ya utekelezaji wa kazi katika eneo lake na kuhamasisha wananchi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umasikini na kuongeza uzaishaji mali.
vii. Kiongozi wa wakuu wa vitengo vya kitaalama katika kijiji.
viii. Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi Kumbukumbu zote na nyaraka za kijiji.
ix. Mwenyekiti wa kikao cha wataalam waliopo katika kijiji,
x. Kupokea, kusikiliza na kutatua malalamiko na migogoro ya wananchi
xi. Kusimamia utungaji wa sheria ndogo za kijiji na;
xii. Kuwa chini Mtendaji wa Kata.
QUALIFICATION AND EXPERIENCE
Kuajiriwa mwenye Elimu ya kidato cha Nne (IV) au cha Sita (VI), aliyehitimu mafunzo ya Astashahada/cheti au NTA level 5 katika moja ya fani zifuatavyo; Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya Sanaa katika Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.
APPLICATION TIMELINE: 2024-07-31 2024-08-09
.