Crude Oil Pipeline-EACOP

OMBI LA KUONESHA NIA YA UBORESHWAJI WA SEKTA YA USHIRIKISHWAJI KWA KUTOA NA KUENDESHA GARI LA MATANGAZO NA KITUO KINACHOTEMBEA CHA HUDUMA YA USHIRIKISHWAJI WA JAMII: KUMBUKUMBU NA. REQ-00000055

WhatsApp
Twitter
Email
LinkedIn
Instagram

Ombi la kuonesha nia ya uboreshaji wa sekta ya ushirikishwaji kwa kutoa na kuendesha gari la
matangazo na kituo kinachotembea cha huduma ya ushirikishwaji wa jamii.
Kampuni ya Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) LTD (EACOP LTD)
inakaribisha kampuni zenye uzoefu na weledi wa kutosha kuonesha nia ya kutoa na kuendesha gari la Matangazo [‘popup truck’) ili kusaidia utekelezaji wa uboreshaji wa sekta na shughuli za
Ushirkishwaji wa Jamii katika wilaya 27 na vijiji 231 vilivyopo katika mkuza wa bomba la mafuta.
Mradi wa EACOP unajumuisha ujenzi na uendeshaji wa bomba la kusafirisha Mafuta lililofukiwa
chini ya ardhi linalokatisha mipaka ya nchi mbili litakalo safirisha mafuta ghafi kwenda kwenye
masoko ya kimataifa. Bomba litaanzia Kabaale katika Wilaya ya Hoima, nchini Uganda, mpaka
rasi ya Chongoleani karibu na Tanga nchini Tanzania. Urefu wa bomba ni kilomita 1,443, kati yake
kilomita 1,147 zitakuwa nchini Tanzania.
MAELEZO MAFUPI YA HUDUMA
Kwa niaba ya KAMPUNI, mkandarasi atakayeteuliwa atatoa huduma ya Kulisimamia na
kuendesha gari la matangazo ya kidijitali ambalo litalenga kukuza ushirikishwaji na ushiriki wa
jamii katika ngazi ya mkoa, wilaya na kijiji katika shughuli za EACOP. Kituo cha Ushirikishwaji
kinachotembea kitatumika katika shughuli zilizoorodheshwa hapa chini:
 Ushirikishwaji wa kila robo mwaka na jamii ya wagavi katika ngazi ya mkoa na wilaya
(kwa mfano: warsha za wagavi, vipindi vya utoaji wa taarifa, n.k.
 Matukio ya ushirikiano na wakandarasi Wakuu wa KAMPUNI pamoja na jamii ya
wafanyabiashara wenyeji.
 Kusaidia usajili wa wagavi wa ngazi ya wilaya kwenye mfumo wa LSSP, n.k.
 Kutoa mafunzo ya muda mfupi kati ya siku 1 hadi 21 kwa jamii ya wafanyabiashara
wenyeji ili kuwajengea uwezo katika utoaji wa huduma na ujuzi wa kisekta

 Shughuli za kujenga uelewa wa jamii zinazohusiana na sera ya EACOP ya usalama, afya,
ulinzi n.k. pamoja na ushirikishwaji mwingine wa jamii unaohusiana na Mradi wa EACOP
unaofanywa na idara mbalimbali za EACOP
Makampuni yanayohitaji yanaweza kushiriki katika wito huu kama kampuni moja moja au
muungano wa Makampuni.
VIGEZO MUHIMU:
Makampuni au taasisi zinazoonesha nia zinaalikwa kutuma maombi na kuambatanisha nyaraka
zifuatazo:
 Leseni ya Biashara.
 Leseni ya biashara kutoka nchii husika inayothibitisha kufanya kazi hii.
 Uthibitisho wa usajili wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na cheti cha uthibitisho wa
mlipa kodi kwa mwaka wa fedha uliopita.
 Inashauriwa kuwasilisha maombi ya usajili kwenye kanzi data ya EWURA ya Watoa
Huduma ya Ugavi wa Ndani [LSSP) wakati wa kuonesha nia.
 Kuzingatia kanuni za watoa huduma wa ndani za mwaka 2017 na ufafanuzi wa makampuni
ya ndani.
 Wasifu wa watendaji watakaohusika katika Mradi ikiwa ni pamoja na nakala za vyeti vyao,
kiwango cha elimu, uzoefu na uwezo wa kutoa huduma inayohitajika.
 Uzoefu, utendaji na uwezo wa kutoa huduma zilizoorodheshwa hapo juu katika kiwango
kikubwa nchini Tanzania, kulingana na viwango vya kitaifa na kimataifa.
 Uwezo wa kifedha wa kutoa huduma zinazohitajika ikiwa ni pamoja na kuwasilisha hesabu
za fedha za miaka mitatu iliyopita.
 Uthibitisho kutoka kwenye mfumo wa Usimamizi wa QHSE, taasisi na mchakato kulingana
na Viwango vya Ndani na vya Ki-Sekta vinavyotumika kwa kazi hii.
 Uthibitisho wa kukubaliana na sera za kupinga rushwa, ufisadi, na Haki za Binandamu.
Makampuni yenye nia, ambayo yana uwezo na rasilimali za kutosha kutoa huduma zilizotajwa
hapo juu yanapaswa kutuma maombi na kuambatanisha nyaraka zilizotajwa hapo juu kupitia barua
pepe ya. [email protected] (ukubwa wa barua pepe usizidi 20Mb) mnamo au kabla ya
Tarehe 15 Disemba 2022 saa 11:00 jioni saa za Afrika Mashariki (EAT). Kichwa cha Barua pepe
kiwe [REQ-00000055] POP-TRUCK.
Maombi yote yakuonesha nia yawe kati ya kurasa 10 hadi 20.
Maombi yote lazima yawasilishwe kwa lugha ya Kiingereza.

Muhimu: EACOP itapitia na kuchambua nyaraka zilizotumwa na makampuni yaliyoonesha nia
kulingana na EOI hii, na kisha kufanya tathmini kulingana na vigezo vya ndani vya EACOP Ili
kubaini makumpuni yenye sifa yatakayojumuishwa kwenye orodha ya awali ya makampuni yenye
vigezo. Mwaliko kwa Makampuni kutuma maombi ya zabuni utatumwa kwa Makampuni ya Awali

yenye vigezo baada ya makampuni hayo kusaini Makubaliano ya Utunzaji wa Taarifa (NDA).
Kampuni ya EACOP LTD ina haki ya kuteua au kukataa kampuni na kubaki na maamuzi yake bila
ya kutoa sababu kwa kamapuni husika.

WhatsApp
Twitter
Email
LinkedIn
Instagram

Related