Crude Oil Pipeline-EACOP

OMBI LA KUONESHA NIA YA UTOAJI WA HUDUMA YA USIMAMIZI WA WAKUFUNZI WAKATI WA PROGRAMU YA MAFUNZO

WhatsApp
Twitter
Email
LinkedIn
Instagram

KUMBUKUMBU NA. 00000240

Kampuni ya Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) Ltd, (“EACOP LTD”)
inakaribisha kampuni zenye uzoefu na weledi wa kutosha ili kuonesha nia ya kutoa Huduma za
Usimamizi wa Mafunzo kwa Wakurufunzi katika kipindi cha programu ya mafunzo.

Mradi wa EACOP unajumuisha ujenzi na uendeshaji wa bomba la kusafirisha Mafuta ghafi
lililofukiwa chini ya ardhi linalokatisha mipaka ya nchi mbili kwa ajili ya kusafirisha mafuta ghafi
kwenda katika masoko ya kimataifa. Bomba litaanzia Kabaale katika Wilaya ya Hoima, nchini
Uganda, mpaka rasi ya Chongoleani, karibu na mji wa Tanga, nchini Tanzania. Urefu wa bomba ni
kilomita 1,443, kati yake kilomita 1,147 zitakuwa nchini Tanzania.

MAELEZO MAFUPI KUHUSU MAWANDA YA HUDUMA
Kwa niaba ya EACOP Ltd, mkandarasi atakayechaguliwa, atasimamia wakurufunzi ambao
watapatiwa mafunzo ya kiufundi kwa awamu mbalimbali kwenye vituo vya mafunzo
vilivyochaguliwa. Programu ya mafunzo itaendeshwa kwa kipindi cha kati ya miezi 24 hadi 30.
Mkandarasi aliyechaguliwa atatekeleza shughuli za usimamizi kwa wakurufunzi zikiwemo
shughuli mahususi zifuatazo:

  • Kufanya tathmini na mapatio ya utimamu au uimarifu wa afya pale inapohitajika na EACOP Itd hii haitajikita kwenye upimaji wa utimamu au uimarifu wa afya tu, bali pia vya kiafya.
  • Kuhakikisha kuwa wakati wote wa mkataba, Wakurufunzi wanaopatiwa mafunzo wanakuwa na maadili mema na afya njema pamoja na uwezo mzuri wa kumudu kutekeleza majukumu yao.
  • Kutoa huduma za usimamizi na uratibu, ambazo zinajumuisha usafirishaji, huduma za matibabu kwa wakurufunzi pamoja na maadili mema na afya ya kimwili, pamoja na uidhinishaji wowote wa kiutawala unaojumuisha vibali vya kazi, na/au viza za kikazi zinazohitajika.
  • Kulipa mshahara wa kila mwezi, posho, tozo zinazotakiwa pamoja na bima, kwa ujumla kulipa gharama zote za moja kwa moja au zisizo za moja kwa moja zinazowahusu wafanyakazi waliotajwa, pamoja na gharama mbalimbali za Kodi na ushuru husika.
  • Kuandaa mahitaji ya safari kwa ajili ya wakurufunzi pale inapohitajika.
  • Kutoa wafanyakazi wenye sifa stahiki kwa nafasi mbili za Mshauri wa Wanafunzi na Msaidizi wa Masuala ya Kiutawala. Wote watafanya kazi mahali ambapo mafunzo yatakuwa yanafanyika.
  • Kutoa vifaa vya Teknolojia ya Mawasiliano kwa WAKURUFUNZI kwa kuzingatia viwango na mahitaji ya EACOP ltd.

VIGEZO MUHIMU:
Makampuni au taasisi zinazoonesha nia zinakaribishwa kutuma maombi na kuambatanisha
nyaraka zifuatazo

  • Leseni ya biashara.
  • Leseni halali, kama ipo, kutoka mamlaka ya ndani ya nchi husika kwa ajili ya utoaji wa
  • huduma husika.
  • Uthibitisho wa usajili wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), na Cheti cha Uthibitisho wa Mlipa Kodi kwa mwaka wa fedha uliopo.
  • Cheti cha usajili au maombi yaliohidhinishwa ya usajili kwenye kanzi data ya Watoa Huduma ya Ugavi wa Ndani (LSSP) ya EWURA wakati wa kuonesha nia.
  • Kukidhi vigezo vya Kanuni ya Maudhui ya Wazawa za mwaka 2017
  • Wasifu wa wafanyakazi muhimu watakaohusika katika mradi ikiwa ni pamoja na vyeti vya lazima vya wahudumu na viwango vya elimu, pamoja na uzoefu na uwezo wa kutoa huduma zinazotakiwa
  • Nyaraka zinazoonesha uzoefu, utendaji na uwezo wa kutoa Huduma kwa maeneo yaliyoorodheshwa hapo juu katika kiwango kikubwa nchini Tanzania, kulingana na viwango vya kitaifa na kimataifa.
  • Uwezo wa kifedha wa kutoa huduma zinazohitajika ikiwa ni pamoja na kuwasilisha hesabu za fedha za miaka mitatu iliyopita
  • Uthibitisho kutoka kwenye mfumo wa Usimamizi wa QHSE, taasisi na mchakato kulingana na Viwango vya Ndani na vya Ki-Sekta vinavyotumika kwa kazi kama hii.
  • Uthibitisho wa sera za kupinga rushwa, ufisadi, na kuzingatia Haki za Binandamu

Makampuni yenye nia, uwezo na rasilimali za kutosha kutekeleza shughuli zilizotajwa hapo juu
yanatakiwa kutuma maombi pamoja na kuambatanisha nyaraka zilizotajwa hapo juu kupitia barua
pepe ya [email protected] , (ukubwa wa barua pepe usizidi 20Mb). Maombi yatumwe
ifikapo au kabla ya saa 11:00 jioni kwa saa za Africa Mashariki (EAT) ya mnamo tarehe 21 Juni2023 Kichwa cha Barua pepe kiwe: 00000240 – Utoaji wa Huduma za Wakurufunzi wa Utawala. Maombi yote ya kuonesha nia yawe kati ya kurasa 10 hadi 20 Maombi yote lazima yawasilishwe
kwa lugha ya Kingereza.

Muhimu: Kampuni ya EACOP LTD itapitia na kuchambua nyaraka zilizotumwa na makampuni
yenye nia kulingana na EOI hii na kisha kufanya tathmini kwa kutumia vigezo vya ndani ili
kubaini makampuni yatakayojumuishwa kwenye orodha ya (Makampuni) ya awali yaliyokidhi
vigezo. Kampuni zilizofuzu hatua ya awali pekee ndizo zitapokea mwaliko wa zabuni, kwa kutia
saini Mkataba wa Kutunza Siri (NDA), kama mwendelezo wa wito wa mchakato wa utoaji wa
zabuni. Kampuni ya EACOP LTD inayo haki ya kufanya maamuzi yake ya kuchagua au kukataa
kampuni na kuheshimu maamuzi yake pasipo kutoa sababu kwa kampuni husika.


WhatsApp
Twitter
Email
LinkedIn
Instagram

Related