LOGO

Tahadhari kwa Taasisi za Serikali, Binafsi na Umma Kuhusu Makampuni Ambayo Hayajahuisha (update) Taarifa zake kwa Mujibu wa Sheria

WhatsApp
Twitter
Email
LinkedIn
Instagram

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA

WAKALA WA USAJILI WA BIASHARA NA LESENI

TAHADHARI KWA TAASISI ZA SERIKALI, BINAFSI NA UMMA KUHUSU MAKAMPUNI AMBAYO HAYAJAHUISHA (UPDATE) TAARIFA ZAKE KWA MUJIBU WA SHERIA

Dar es Salaam, Desemba 19, 2020

Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) unapenda kutoa tahadhari kwa Wizara,Mamlaka, Taasisi za Serikali, Taasisi Binafsina Umma kwa ujumla kuhusu uwepo wa Makampuniambayo hayajahuisha (update) taarifa zake kwa Mujibu wa Sheria.

Kwa taarifa hii, Umma unahimizwa kuhakikisha Mikataba yote ya manunuzi ya vifaa au huduma (All kinds of contractual transactions} baina yao na Kampuni binafsi isainiwe baada ya kujiridhisha kwamba Kampuni husika imehuisha taarifa zake za mwaka katika Daftari la Makampuni kama yalivyo matakwa ya Sheria na kama kampuni hizo bado ziko hai. Kujiridhisha huko kufanyike kwa Kampuni husika kutakiwa kuwasilisha Cheti cha Usajili (Certificate of Incorparation) na nakala ya Mizania yake ya Mwaka huo (Annual returns) iliyoidhinishwa na Msajili wa Makampuni au Taarifa Rasmi (Official Search Report) iliyosainiwa na Msajili wa Makampuni.

BRELA inapenda kukumbusha Umma kuwa, kwa mujibu wa kifungu cha 128 cha Sheria ya Makampuni, Sura 212 kila Kampuni iliyosajiliwa hapa nchini (Locally Registered Company) inapaswa kuwasilisha kwa Msajili wa Makampuni Taarifa za Mwaka (Annual Returns) na kwa upande wa Kampuni zilizosajiliwa nje ya nchi (Companies incorporated outside Tanzania) na kufungua tawi hapa nchini, huwasilisha Mahesabu ya Mwaka (Annual Accounts) kwa mujibu wa kifungu cha 438 cha Sheria ya Makampuni, Sura 212.

Izingatiwe kwamba, Taarifa ya mwaka husaidia kutoa taswira halisi ya Kampuni na hivyo kusaidia mtu yeyote anayetaka kuingia makubaliano ya kibiashara na Kampuni husika kufanya maamuzi stahiki na kufahamu ni nani haswa wanahusika na utiaji saini wa mikataba.

BRELA inatoa rai kwa Wizara, Mamlaka, Taasisi za Serikali, Taasisi Binafsi na Umma kwa ujumla kuchukua tahadhari dhidi ya kampuni ambazo hazija huisha taarifa zake kwa mujibu wa Sheria, hii itasaidia kuepusha madhara ya kisheria na kiuchumi yanayoweza kujitokeza kwa kufanya kazi na kampuni ambayo haijahuisha taarifa zake kwa Msajili wa Makampuni.

“Tunaipa utu wa kisheria biashara yako”

Imetolewa na: i

AFISA MTENDAJI MKUU

WAKALA WA USAJILI WA BIASHARA NA LESENI

WhatsApp
Twitter
Email
LinkedIn
Instagram

Related