TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI

WhatsApp
Twitter
Email
LinkedIn
Instagram

 

TO JOIN OUR TELEGRAM GROUP CLICK HERE

TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) anapenda kuwataarifu Waombaji wote wa kazi zilizotangazwa kupitia tangazo lenye Kumb. Na. CA.37/476/01 la tarehe 12 Juni, 2022, kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 11 Julai, 2022 hadi tarehe 12 Julai, 2022 katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya na hatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi watakaofaulu usaili huo. Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-
1. Usaili wa mtihani wa kuandika (written interview) utafanyika tarehe 11 Julai, 2022 saa 1:00 kamili asubuhi.

2. Usaili wa vitendo na mahojiano ya ana kwa ana (Practical and Oral Interview) utafanyika tarehe 12 Julai, 2022 saa 1:00 kamili asubuhi.

3. Kila msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi.

4. Vitambulisho vitakavyokubalika siku ya usaili ni pamoja na:- Kitambulisho cha mkazi, Kitambulisho cha Mpiga kura, Kitambulisho cha uraia (NIDA) au Hati ya kusafiria.

5. Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha kuzaliwa, kidato cha IV, Kidato cha VI na Shahada kutegemeana na mahitaji ya tangazo la kazi na sifa za Mwombaji.

6. Wasailiwa watakaowasilisha Testimonials; Matokeo ambayo hayajakamilika (Provisional Statement of Results) au hati za matokeo za kidato cha IV na VI (Results Slips) HAVITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI.

7. Kila msailiwa atajigharamia kwa chakula, usafiri na malazi.

8. Kwa waomba waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na mamlaka husika (TCU, NACTE au NECTA).

DOWNLOAD PDF HERE

WhatsApp
Twitter
Email
LinkedIn
Instagram

Related