TASAF

TANGAZO LA MNADA WA HADHARA WA MAGARI CHAKAVU

WhatsApp
Twitter
Email
LinkedIn
Instagram

TANGAZO LA MNADA WA HADHARA WA MAGARI CHAKAVU

i. Wananchi wote mnatangaziawa kwamba Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) ikishirikiana na Ofisi ya Msimamizi Mkuu wa Mali za Serikali Mkoa wa Dar es Salaam itaondosha kwa njia ya mnadawa hadhara Magari Chakavu yaliyoko Ofisi za TASAF – Dare es Salaam siku ya Jumatano tarehe 7/09/2022.

ii. Magari yatakayouzwa ni kama ifuatavyo:

iii. Masharti ya Mnada:-

a) Magari yatauzwa kama yalivyo.

b) Mnunuzi atatakiwa kulipia asilimia 25% ya bei aliyoshinda mara tu baada ya dalali kumtangaza mshindi na kiasi kinachobaki kilipwe katika kipindi cha siku 14 kutoka tarehe ya mnada, Ikiwa mnunuzi atashindwa kulipa kiasi fedha iliyobaki, kiasi alicholipa awali hakitarudishwa.

c) Mtu yeyote atakae tamka bei ya juu kisha akashindwa kulipa asilimia ishirini na tano(25%) ya bei aliyotamka atachukuliwa kuwa ni mwenye kutaka kuvuruga Mnada na hivyo hatua kali zakisheria zitachukuliwa juu yake kwa mujibu wa sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

d) Mnunuzi atatakiwa kuondoa /kuchukua gari alilonunua ndani ya siku saba (7) kuanzia siku ya kukamilisha malipo.

e) Gharama za kubadilisha umiliki ni jukumu la mnunuzi na atatakiwa kukamilisha taratibu za kumilikishwa kwa mujibu wa sheria ndani ya siku ishirini na moja(21).

 f) Wanaopenda kuona magari hayo wataruhusiwa kufanya hivyo siku mbili (2) kabla ya mnada.

 g) Mnada utaanza saa nne(04:00)kamili katika maeneyo ya Ofisi za TASAF Dare es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji

Mfuko wa Maendeleo ya Jamil – TASAF

Barabara ya Jakaya Mrisho Kikwete

S.L.P. 2719 Dodoma, Tanzania i.

Simu: 255 026 2983866 8

Nukushi: 265 026 2963871

Barua pepe: [email protected]

WhatsApp
Twitter
Email
LinkedIn
Instagram

Related