JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA UJENZI NA UCHUKUZI
WAKALA YA BARABARA TANZANIA
Wananchi wote mnatangaziwa kwamba Serikali,kupitia Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Morogoro itauza kwa njia ya mnada wa hadhara vifaa chakavu vya aina mbalimbali vya ofisini na majumbani.
VIFAA VITAKAVYONADIWA:
i) Samani za aina mbalimbali (meza, makochi,vitanda na kadhalika ).
ii) Vifaa Vingine (Majiko ya Umeme & Mitungi ya Gesi, majokofu na kadhalika).
MAHALI:
Ofisi ya Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Morogoro.
MUDA:
Mnada utaanza saa 3:00 (saa tatu kamili) asubuhi.
Masharti ya mnada:
Watakaopenda kuona vifaa hivyo wataruhusiwa kufanya hivyo siku moja kabla ya siku ya mnada.
Tafadhali kumbuka kuwa vifaa vinauzwa kama vilivyo na mahali vilipo. Vifaa husika ni kama _ ilivyoonyeshwa kwenye jedwali lililoambatanishwa na tangazo hili.
Imetolewa na;
KAIMU MENEJA WA MKOA,
WAKALA YA BARABARA TANZANIA,
S.L.P 91,
MOROGORO.

Mtaa wa Simba. S.L.P 91, Morogoro, Simu: +255 23 2935223/4, Nukushi +255 23 2935224/5,
Barua pepe [email protected]