wakala misitu

Tangazo la Uuzaji Wa Miti Ya Misaji Iliyopandwa Kwenye Mipaka Ya Misitu Ya Hifadhi Kwa Njia Ya Mnada Katika Wilaya Ya Muheza Na Hifadhi Ya Mazingira Asili Nilo (Korogwe)

WhatsApp
Twitter
Email
LinkedIn
Instagram

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII

WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU TANZANIA

TANGAZO

UUZAJI WA MITI YA MISAJI ILIYOPANDWA KWENYE MIPAKA YA MISITU YA HIFADHI KWA NJIA YA MNADA KATIKA WILAYA YA MUHEZA NA HIFADHI YA MAZINGIRA ASILI NILO (KOROGWE)

1. Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) unatarajia kuuza miti aina ya Misaji yenye jumla ya meta za ujazo 1,600.883 zilizopandwa kwenye mipaka ya misitu ya hifadhi katika Wilaya ya Muheza na Hifadhi ya Mazingira AsiliaNILO. Uuzaji huu utafanyika kwa njia ya mnada (Auction) kwa kuzingatia kifungu cha ya 31 (ii) cha kanuni za sheria ya Misitu za mwaka 2004. Mnada utafanyika tarehe 13 Agusti, 2019 katika ofisi ya Misitu Wilaya ya Tanga Saa Tano kamili (5.00) Asubuhi. Miti hii ya misaji itauzwa mahali ilipo na jinsi ilivyo na mnunuzi hatakuwa na haki ya kudai fidia baada ya mauzo.

2. Kampuni au mtu binafsi anayetaka kushiriki mauzo kwa njia ya mnada
anatakiwa kuwasilisha maombi kwenye bahasha iliyofungwa kuonesha nia ya kushiriki mauzo kwa njia ya mnada akiambatanisha, usajili wa kiwanda cha kupasua magogo (Mwaka 2019/2020) na cheti cha utambulisho wa mlipa kodi (TIN). Aidha, anatakiwa aoneshe jina la msitu wa hifadhi, bei na ujazo anaotarajia kununua kwa kuzingatia miti iliyopandwa kwenye mipaka ya misitu ya hifadhi kama inavyobainishwa kwenye Jedwali Namba 1.

3. Mnada utaendeshwa hadharani wakiwepo wanunuzi wote katika ofisi ya
Misitu Wilaya ya Tanga Mtaa wa Chumbageni jijini Tanga siku ya Jumanne
tarehe 13 Augusti, 2019 kwa kufuata sheria ya misitu Sura 323. Aidha miti
iliyopandwa kwenye mpaka wa kila Msitu wa Hifadhi itanadiwa peke yake
kulingana na bei na ujazo uliopo. Hata hivyo bei ya juu iliyotolewa na
mnunuzi wakati wa kufungua bahasha haitazuia wanunuzi wengine kuongeza bei zaidi ya iliyotajwa awali. Mnunuzi atakayetoa bei ya juu atatakiwa IA

malipo kama ilivyoainishwa hapo chini kifungu namba 10. Baada ya malipo
atasaini mkataba wa mauzo na Wakala wa kumruhusu kuvuna miti hiyo.

4. Wakala wa huduma za Misitu Tanzania unawaalika wanunuzi kutuma
maombi yao kwa ajli ya kununua miti ya misaji kwa njia ya mnada ambapo mnunuzi anaweza kuchagua mojawapo kati ya mipaka ya misitu ya hifadhi yenye miti ya misaji kama ifuatavyo:

NA Jina la Msitu wa Hifadhi Wilaya LOT No. Ujazo wa miti iliyopo kwenye mpaka wa msitu (m3 ) Bei pendekezi
1 Kwani Muheza I 602.89 415,000/=
2 Tongwe Muheza II 631.20 415,000/=
3 Nilo Jr Korogwe III 366.793 450,000/=
  Jumla                                                                                                             1,600.883  

5. Wakala wa huduma za misitu Tanzania utatoa hati ya ushindi kwa mnunuzi aliyetaja kiwango cha juu cha bei kwa kila ujazo wa miti ya misaji iliyopo kwenye mpaka wa misitu ya hifadhi katika jedwali Na.1.


6. Mnunuzi atakayefanikiwa kununua miti ya misaji hataruhusiwa kusafirisha magogo nje ya nchi isipokuwa baada ya kuchakata kwa mujibu wa kifungu cha 50 (1) cha kanuni za misitu za mwaka 2004 na Tangazo la Serikali
Na.69 la Mwaka 2006.

7. Makampuni na watu binafsi wanakaribishwa kutembelea mipaka ya misitu yenye miti ya misaji wakati wa saa za kazi kuanzia saa mbili (2.00) asubuhi hadi saa tisa na nusu (9.30) alasiri isipokuwa siku za mapumziko. Meneja wa Misitu Wilaya ya Muheza au msaidizi wake atakuwepo kwa ajili ya maelekezo zaidi.

8. Wanunuzi wanapaswa kuchukua na kusoma masharti ya uvunaji wa miti ya misaji iliyopandwa kwenye mipaka ya misitu ya hifadhi ili kuepuka uharibifu wa misitu ya asili wakati wa uvunaji.

9. Kiwango cha juu cha bei kwa kila ujazo atakachotoa mteja kitajumuisha
VAT, CESS, TaFF, Forest Royalty pamoja, na gharama za upandaji miti.

10. Mnunuzi atakayeshinda atalipa asilimia ishirini na tano (25%) ya thamani yote ya ununuzi siku tatu (3) baadaa ya mnada kufanyika. Fedha hizo hazitarudishwa endapo mhusika atashindwa kukamilisha asilimia 75% iliyobaki ndani ya siku kumi na nne (14). Asilimia sabini na tano (75%)
iliyobaki italipwa ndani ya siku kumi na nne (14) baada ya mnada .Malipo
yote yafanyike kwa kupitia mfumo wa makusanyo ya serikali (GePG) baada
ya kupewa Bill. Hati ya madai inayoonesha kiasi cha kulipa itatolewa na
meneja wa Misitu Wilaya ya Muheza na muhifadhi wa Mazingira Asilia-Nilo

11. Mnunuzi atapaswa kuwasilisha hati ya malipo kwa Meneja wa Misitu
Wilaya ya Muheza kama uthibitisho wa malipo siyo zaidi ya siku tatu (3)
baada ya malipo kufanyika.

12. Wanunuzi watakaoshinda watasaini mkataba na kupewa leseni ya
kuvuna miti ya misaji na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania ndani ya
siku saba baada ya kukamilisha malipo ya gharama zote kwa asilimia 100% na atatakiwa kuondoa mazao yake katika kipindi cha mwezi mmoja baada
ya kupewa leseni.

13. Maombi yote yawasilishwe siku ya mauzo kabla ya saa 4.30 asubuhi.
Aidha wanunuzi watakaochelewa kuwasilisha maombi yao kwa siku na
muda uliopangwa hawataruhusiwa kushiriki katika mnada.

Tangazo hili pia linaweza patikana katika tovuti zifuatazo www.tfs.go.tz na www.mnrt.go.tz]

Imetolewa na:
MTENDAJI MKUU
WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU TANZANIA
S.L.P 40832
DAR ES SALAAM
SIMU NA. : (+255) (022) 2864249
NUKUSHI : (+255) (022) 2864257
BARUA PEPE: [email protected]

MNADAMUHEZA-NAKOROGWE-WAKALA-WA-HUDUMA-ZA-MISITUDownload
WhatsApp
Twitter
Email
LinkedIn
Instagram

Related