LOGO

Tangazo la Zabuni Halmashauri ya Jiji la Tanga

WhatsApp
Twitter
Email
LinkedIn
Instagram

HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA

TANGAZO LA MARUDIO YA ZABUNI

1. Halmashauri ya Jiji la Tanga katika mwaka wa Fedha 2019/2020
ina mipango mbalimbali ya kuboresha ustawi wa maisha ya
wananchi wa MkoawaTanga na Watanzania kwa ujumla imekuwa
ikitoa fursa sawa kwa wananchi wa jinsia zote kujipatia maeneo ya
kufanyia biashara katika masoko na majengo yake kwa utaratibu
wa upangishaji na ukusanyaji wa Ushuru wa mapato kupitia
wafanyabiashara/Makampuni/Ushirika/Vikundi kwa niaba ya
Halmashauri ili waweze kufanya biashara kwa nia ya kujipatia
kipato na ajira.

Halmashauri ya Jiji la Tanga inawatangazia wadau wote Zabuni
zifuatazo:-

Na. ZABUNI Na MAELEZO ENEO/SEHEMU HUSIKA
1 LGA/128/2019- 2020/HQ/NC/01 Wakala wa ukusanyaji wa Ushuru wa Mapato. Choo cha Soko la Kisosora, Choo cha Soko la Mkwakwani,choo cha bustani ya Sakarani, choo cha Soko la Majengo, choo cha gulio la Tangamano na Ushuru wa Samaki vituo vya kukusanyia Samaki Kasera na Mchukuuni.
2 LGA/128/2019- 2020/HQ/NC/02 Upangishaji wa maeneo mbalimbali ya biashara ikiwemo :-Maduka, Bucha Vizimba na Ofisi Soko la Mgandini, b Makorora, Mlango Chuma,Ngamiani, Mkwakwani, Tangamano Community Centre, Soko la Majengo na Bustani ya Jet.

2. Kabrasha za Zabuni zinapatikana ofisi ya Ununuzi ya Jiji la Tanga,
Chumba Na.6, gharama za kununua Zabuni ni Tshs. 50,000 kwa
zabuni za ukusanyaji Ushuru,Maduka/mabucha/Ofisi na Store
Tshs. 20,000/= na kwa vizimba vya mboga/matunda na wafanya
biashara wa jua kali Tshs. 5,000/= ambazo hazitarajeshwa.
Maombi ya Zabuni yatumwe kwa kupitia anuani ya Mkurugenzi
wa Jiji, S.L.P. 178, Tanga na yawasilishwe Ofisi za Jiji la Tanga kwa
Katibu wa Bodi ya zabuni Chumba Na. 6.

3. Halmashauri inapenda kuwasisitiza Wadau/Wananchi wake wote
waliopo katika maeneo yake mbalimbali ya upangishaji wenye
nia ya kuendelea kupanga wahakikishe wanaomba upya maeneo
hayo ili kuepuka usumbufu.

4. Mwisho wa kutuma maombi ni Jumatano saa 4.00 Asubuhi
tarehe 14/08/2019 ambapo yatafunguliwa muda mfupi baadaye.
Maombi (Zabuni) yatakayowasilishwa baada ya saa nne Asubuhi
tarehe 14/08/2019 hayatafikiriw
a.

5. Kwa maelezo zaidi fika Ofisi za Jiji la Tanga – Kitengo cha Ununuzi au wsiliana kwa barua pepe [email protected]

kaz. Ramadhani Possi
KAIMU MKURUGENZI WA JIJI
TANGA

WhatsApp
Twitter
Email
LinkedIn
Instagram

Related