HALMASHAURI YA WILAYA YA SAME
TANGAZO LA ZABUNI
Halmashuri ya wilaya ya Same inatoa tangazo la zabuni ya kuodishaji wa vibanda vipya vilivyopo kituo cha mabasi Same Mjini
Aidha halmashauri ya wilaya inakaribisha maombi kwaajili ya kutoa huduma mablimbali kam ilivyoaniskwa kwenye jedwali hapo chini
Tangazo hili la zabuni liko wazi kwa watu binafsi, kampuni na taasisi yoyote iliyosajiliwa kisheria kufanya biashara kutoa huduma kama hii
1 | Ukodishaji wa vibanda Block (F) 2 | LGA/049/NC/block .F/2019/2020/07 |
2 | Ukodishaji wa vibanda Block (A) 3 | LGA/049/NC/block .A/2019/2020/08 |
3 | Ukodishaji wa vibanda Block (B) 2 | LGA/049/NC/block .B/2019/2020/09 |
4 | Ukodishaji wa mgahawa Halmashauri ya Wilaya ya Same | LGA/049/NC/ 2019/2020/10 |
5 | Ukodishaji bar Padeco Same Mjini | LGA/049/NC/ 2019/2020/11 |
6 | Unyonyaji maji taka | LGA/049/NC/ 2019/2020/12 |
SIFA NA MASHARTI KWA MUOMBAJI
- Mwombaji ni lazima ataje bei ya pango kwa mwezi atakayolipa kwa vibanda, ukodishaji wa mgahawa na bara Padeco
- Mwombaji ataje kibanda anachoomba mfano Kibanda Block A,B,F
- Mwombaji aambatanishe hati ya usajili extract register au memorandum of association picha za wakurugenzi wamiliki iwapo mwombaji ni kampuni , kikundi au shirika
- Mwombaji binafsi aambataishe picha yake katika maombi na igongwe muhuri na afisa mtendaji Kijiji/kata pamoja na barua ya utambulisho kutoka kwa afisa mtendaji kata/kijiji
- Mwombaji binafsi aambtanishe nakala ya kitambulisho cha kupigia kura au kitambulisho cha taifa pamoja na nakala ya cheti cha utambulisho wa mlipa kodi (TIN Certificate) na leseni iliyo hai
- Mwombaji ataje aina ya biashara atakayofanya katika kibanda kinachopangishwa
- Mwombaji lazima awe Mtanzania
- Mwombaji wa huduma ya maji taka lazima aambatanishe kibali za baraza la mazingira
- Ada ya maombi ya zabuni ni 30,000/= fedha ambazo hazitarejeshwa
- Kitabu cha zabuni kinapatikana ofisi ya kitengo cha manunuzi chumba na 502
- Watumishi wa Halmashsuri ya wila ya same hawataruhusiwa kushiriki katika zabuni hii
NAMNA YA KUTUMA MAOMBI
Maombi yote yafungwe kwenye bahasha kwa kutumia lakiri(seal) na isionyeshe alama yoyote toka kwa mwombaji na ndani ya bahasha iambatanishwe stakabadhi ya malipo ya ada ya maombi ya zabuni pamoja na hati mbalimbali zenye kutambulisha mwombaji . juu ya bahasha yenye maombi paandikwe kwa herufi kubwa jina la zabuni anayoomba mafano
KWA VIBANDA,
UKODISHAJI WA VIBANDA VLIVYOPO KITUO CHA MABASI SAME MJINI ZABUNI NAMBA LGA/049/block.B/2019/2020/09
UKODISHAJI WA VIBANDA VIPYA (VIDOGO) KITUO CHA MABASI SAME MJINI
Maombi yaumw kwa anuani ifuatayo
KATIBU BODI YA ZABUNI (W),
S.L.P 138,
SAME
Na kutumbukiza kwenye sanduku la zabuni lililopo katika ofisi ya mkurugenzi, siku ya mwihso kuwasilisha maombi ni tarehe 08/07/2020 saa nne asubuhi na ufunguzi wa zabuni hizo utafanyika kuanzia saa 4 asubuhi kaika ukumbi wa halmashuri ya Same
Maombi yatakayochelewa au yaliotumwa kwa fax, telegram hayatafanyiwa kazi
Bodi ya zabuni hailazimiki kukubali zabuni ya juu au ya chini
Chanzo Daily News 24th June 24, 2020