mamcu

TANGAZO LA ZABUNI YA UNUNUZI WA PAMOJA (BULK PROCUREMENT) WA VIUATILIFU, MABOMBA NA MAGUNIA KWA MSIMU WA MWAKA 2022/2023

WhatsApp
Twitter
Email
LinkedIn
Instagram

MASASI MTWARA COOPERATIVE UNION( MAMCU ) LTD
REG. NO 5511 MTR

TANGAZO LA ZABUNI YA UNUNUZI WA PAMOJA (BULK PROCUREMENT) WA VIUATILIFU, MABOMBA NA MAGUNIA KWA MSIMU WA MWAKA 2022/2023

ZABUNI NAMBA: 1. VIUATILIFU/UNIONS/2022
ZABUNI NAMBA: 2. MAGUNIA/UNIONS/2022
ZABUNI NAMBA 3.MAMBOMBA YA UPULIZIAJI/UNION/2022

Tarehe: 25.08.2021

1. Vyama Vikuu vya Ushirika vinavyohudumia wakulima wa zao la Korosho vya TANECU LTD, MAMCU LTD, TAMCU LTD, RUNALI LTD , CORECU LTD na LINDI MWAMBAO LTD vinatangaza zabuni ya ununuzi wa pamoja wa Viuatilifu na Magunia kwa msimu wa 2022/2023.

2. Kwa idhini ya Bodi ya Vyama Vikuu hivyo, Mwenyekiti wa kamati ya zabuni ya ununuzi wa pamoja anatangaza zabuni shindani ya kitaifa (National Competitive Tendering- NCT) ya ununuzi wa Pamoja (Bulk Procurement) ya Viuatilifu kwa ajlli ya maandalizl ya mslmu wa Korosho kwa mwaka 2022/ 2023 kama ifuatavyo: –

3 . Wanakaribishwa Wazabuni wenye uwezo wa kusambaza Viuatilifu, mabomba na Magunia tajwa hapo juu kwenye jedwali

4. Viuatilifu vyote vya Kimiminika/maji viwe katika kifungashio vya ujazo usiozidi Nusu lita

5. Viuatilifu vyote vinapaswa kuwa vimetengenezwa hivi karibuni na lazima viwe angalau na miaka miwili ya Maisha rufani.
6. Mzabuni mmoja anaruhusiwa kuomba LOT zote au sehemuya LOT endapo atakuwa na vigezo stahiki.
7. Mchakato wa Zabuni hii utafanyika kwa njia shindani ya Kitaifa (NCT) kwa mujibu wa Kanuni za Ununuzi wa Umma ya Mwaka 2013 na Marekebisho yake  ya 2016 na ni zabuni ya wazi kwa Wazabuni wote wenye sifa stahiki.

8. Wazabuni wenye nla ya kushlriki, wanakaribishwa ofisi ya Katibu wa Kamati ya Ununuzi wa Pamoja iliyopo wilaya ya Mtwara Mtaa wa barabara ya TANU. Jengo la Ushirikawa Wakulima, Ofisiya MAMCU LTD ghorofa ya pili kwa ajili ya kuchukua Kitabu cha Zabuni (Tender Documents) wakati wa saa za kazi kuanzia saa mbili asubuhi (2:00) hadi saa kumi na nusu jioni (10 :30) isipokuwa siku za Jumamosi na Jumapili pamoja na siku za sikukuu.
9. Kitabu cha Zabuni kitapatikana kwa kuandika barua kwa Katibu wa Kamati ya Ununuzi wa Pamoja ya kuomba kuuziwa Kitabu cha Zabuni (Tender Documents) kwa gharama ya shilingi za kitanzania Laki Mbili (200,000/=) Tu ambazo hazitorudishwa (non-refundable fees) na fedha zote zilipwe kupltia:-

Jina: MAMCU LTD
AkauntiNa: 01J1015468703

BENKI YA CRDB, TAWI LA MTWARA

10. Wazabuni wote wawasilishe Zabuni zao Nakala Tatu [Nakala Halisi moja (original) na Nakala kivuli mbili (kopi)) zikiwa zimefungwa kwa umakini na kutlwa lakiri. Zabuni zote zitafunguliwa mara baada ya muda wa mwisho wakuwasilisha, tukio ambalo litakuwa la wazi na wazabuni au wawakilishi wao wanakaribishwa kuhudhuria. Mwisho wa kupokea na kufungua zabuni ni siku ya Jumatano ya Tarehe 15/09/2021 saa 4:00 Asubuhi katika Ofisi ya MAMCU LTD Mtwara Mjini.

Maombi yatumwe kwa Anuani ifuatayo:-
Katibu wa Kamati ya Ununuzi wa Pamoja,

MAMCU LTD,

S.L.P 660,
Mtwara

Au yapelekwe kwenye ofisi ya Meneja Mkuu wa Chama Kikuu cha Ushirika MAMCU LTD iliyopo Mtwara mjini Jengo la Ushirika wa Wakulima, mtaa wa TANU road.

Meneja Mkuu,

MAMCU LTD,

S.L.P 660,
Mtwara.

11. Zabuni zote sharti ziambatanishwe na dhamana (Bid Security in the form of Bank Guarantee) ya asilimia mbili (2%) ya thamani ya zabuni. Uhai wa dhamana ni siku thelathini (30) baada ya mwisho wa Uhai wa Zabuni.

12. Zabuni zitakazochelewa kupokelewa hazitafikiriwa wakati wa tathmini bila kujall sababu zozote za kuchelewa.

MWENYEKITI WA KAMATI YA UNUNUZI WA PAMOJA

VYAMA VIKUU VYA USHIRIKA WA KOROSHO

WhatsApp
Twitter
Email
LinkedIn
Instagram

Related