LOGO

Tangazo La Zabuni Ya Uwakala Wa Kukusanya Ushuru

WhatsApp
Twitter
Email
LinkedIn
Instagram

Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania,

Ofisi Ya Rais Tawala Za Mikoa Na Serikali Za Mitaa .

HALMASHAURI YA WILAYA TARIME

Tangazo La Zabuni Ya Uwakala Wa Kukusanya Ushuru Zabuni

NA.LGA/067/2020/2021/S/01.

MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA TARIME.
Anapenda Kuwatangazia Wananchi Wote Wenye Sifa Na Uwezo Kutoka Ndani Na Nje Ya Wilaya Ya Tarime Zabuni Za Uwakala Wa Kukusanya Mapato Kwa Kipindi Cha July 2020 -Juni. 2021;
04/06/2020

KWA VYANZO VYA MAPATO VIFUATAVYO:
Soko na Mnada wa Mtana.
• Ushuru wa Magari Mpakani-Sirari
• Ushuru wa Mazao Halmashauri Nzima ya Wilaya na Soko la Sirari.,
HUDUMA YA ULINZI.
• Huduma ya Ulinzi Makao Makuu ya Halmashauri na Nyumba ya Mkurugenzi.

SIFA NA MASHARTI YA MWOMBAJI:-.
• Mwombaji aambatanishe kivuli cha Leseni hai ya biashara Hati ya usajili wa Mlipa kodi (TIN), Pamoja na hati ya usajili iwapo mwombaji ni kikundi, Shirika au Kampuni. Iwapo mwombaji ni mtu binafsi awe Raia wa Tanzania na aambatanishe barua ya utambulisho wake kutoka kwa Mwenyekiti wa Kitongoji na Kijiji pamoja na kivuli cha kitambulisho cha mkazi.
• Mwombaji asiwe anadaiwa na Halmashauri kwa kazi yoyote ile, na awe na uzoefu wa kutosha juu ya kazi anayoomba.
• Pia awe tayari kuheshimu Mkataba endapo atafanikiwa.
• Kubadilisha jina kwa mwombaji anayedaiwa ni udanganyifu usioruhusiwa katika kazi hii. Ikibaini kuwa kuna udanganyifu wa uombaji hatua kali za kisheria zitachukuliwa ikiwa ni pamoja na kufutiwa matokeo.
• Mwombaji atalazimika kulipa kiasi chote cha makusanyo katika akaunti ya Halmashauri na ataje kiwango cha asilimia atakachohitaji kurejeshewa kama gharama za ukusanyanyaji.
• Mwombaji atalazimika kukusanya mapato kwa kuzingatia viwango vya ushuru vilivyowekwa na Halmashauri.
• Mwombaji atalazimika kukusanya mapato kwa kutumia Mashine za kieletroniki (POS) za Halmashauri
• Mwombaji aambatanishe nakala ya taarifa zake za kibenki (Bank Statement) ya kipindi cha miezi sita mfululizo.
• Mwombaji atawajibika kufanya usafi katika eneo atakalopewa kwa gharama zake kwa kipindi chote atakachofanya kazi.
• Mwombaji asiwe Mtumishi au Kiongozi katika Halmashauri ya Wilaya ya TARIME.
• Mwombaji atakayeshinda Zabuni kabla ya kufunga mkataba atalazimika kulipa fedha anayokusudia kukusanya kwa mwezi. Fedha hizi ziwekwe kwenye akaunti ya Amana Namba 30410001498 na kuwasilisha hati ya malipo Halmashauri.
• Mwombaji anatakiwa alipe ada ya maombi ya Tshs. 50,000.00 ambayo hairudishwi. Fedha hizo zitalipwa na kukatiwa stakabadhi ya Halmashauri katika Ofisi ya fedha ya Halmashauri ya Wilaya ya Tarime.
Halmashauri ya Wilaya ya
• Mwombaji atapatiwa Nyaraka za Zabuni kutoka Ofisi ya Katibu wa Bodi ya Zabuni ya Tarime, S.L.P 16, TARIME baada ya kulipa ada ya maombi
• Zabuni hii ipo wazi kwa mtu binafsi, kikundi cha watu kilichosajiliwa Kisheria, Ushirika, Kampuni au Serikali ya Kijiji, ilimradi awe na sifa na uwezo wa kufanya shughuli hizi na awe tayari kuheshimu Mkataba.
• Kila mwombaji atawajibika kutembelea eneo analotarajia kukusanya mapato na kutathimini kwa kina kabla ya kutuma maombi yake na ataje kiasi atakachoweza kukusanya kwa mwezi.
• Mwombaji aambatanishe katika maombi yake tamko la kutojihusisha na vitendo vya Rushwa au ushawishi wa aina yoyote, fomu ya tamko hili imeambatanishwa ukurasa wa mwisho wa kitabu cha zabuni.
• Bodi ya Zabuni haitalazimika kukubali zabuni iliyo juu au chini.
• Mwombaji wa Zabuni ya Ulinzi lazima iwe ni Kampuni Iliyosajiliwa na yenye silaha za moto.

NB: Mwombaji anaruhusiwa kupata ufafanuzi wa sharti lolote asilolielewa kabla ya kutuma maombi yake.

  • UTARATIBU WA KUTUMA MAOMBI:
    Maombi yatumwe kwa anuani ifuatayo.

KATIBU BODI YA ZABUNI HALMASHAURI YA WILAYA YA TARIME S.L.P 16 TARIME.
• Juu kabisa ya Bahasha paandikwe kwa herufi kubwa Zabuni ya Uwakala Wa ……… (Taja aina ya Zabuni unayoomba na katika bahasha hiyo pasionyeshe alama yoyote ya utambulisho wa mwombaji juu ya bahasha pia paandikwe usifungue kabla ya saa 4.30 asubuhi.
• Bahasha ifungwe madhubuti kwa LAKIRI na ndani ya bahasha iambatanishwe stakabadhi halisi ya malipo ya ada ya maombi, malipo ya mwezi Mmoja (1) na vivuli vya leseni,cheti cha usajili wa kampuni ,cheti cha utambulisho wa kampuni kisheria (certificate of incorporation) na hati mbalimbali zenye kutambulisha uhalali wa mwombaji / maombi.
• Nyaraka za maombi ya zabuni ikiwa imeambatanishwa na barua ya maombi itumbukizwe ndani ya sanduku la Zabuni lilipo katika Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji (W) kuanzia saa 2.00 asubuhi hadi saa 9.30 mchana siku za kazi tu. Mwombaji anapaswa kusaini katika kitabu cha kupokelea zabuni
• Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 19/06/2020 Saa 6:00 Mchana siku ya Ijumaa. Zabuni zitafunguliwa siku hiyo hiyo ya mwisho wa kupokea maombi.
• Mwisho wa kupokea Maombi ni Saa 6:00 Mchana, maombi yoyote yatakayowasilishwa baada ya kitabu cha zabuni
• kufungwa yatarudishwa bila kufunguliwa.
• Mwombaji mwakilishi wake anashauriwa kuhudhuria zoezi la ufunguzi litakalofanyika kuanzia Saa 6:00 Mchana katika
• ukumbi wa Halmashauri.
• Uhai wa Zabuni (Tender validity) ni siku 60 baada ya ufunguzi.
• Maombi yaliyochelewa, ambayo hayakusomwa wakati wa ufunguzi au yaliyotumwa kwa Fax, Telex, Telegram au maombi yaliyonakilishwa hayatafikiriwa kwa namna yoyote ile.

APOO C. TINDWA MKURUGENZI MTENDAJI
TARIME

WhatsApp
Twitter
Email
LinkedIn
Instagram

Related