TARURA

Tangazo la Zabuni ya Wakala Utozaji wa Ada za Maegesho ya Vyombo vya Usafiri Kwenye Hifadhi za Barabara za Halmashauri ya Manispaa ya Moshi Mkoa wa Kilimanjaro

WhatsApp
Twitter
Email
LinkedIn
Instagram

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS

TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA WAKALA WA BARABARA ZA VIJIJINI NA MIJINI (TARURA)

MARUDIO YA TANGAZO LA ZABUNI NA AE/092/2019/2020/KLI/NC/01

YA

WAKALA WA UTOZAJI WA ADA ZA MAEGESHO YA VYOMBO VYA USAFIRI KWENYE HIFADHI ZA BARABARA ZA HALMASHAURI YA MANISPAA YA MOSHI MKOA WA KILIMANJARO

1.Wakala wa Barabara za vijijini na mjini Tanzania (TARURA) Mkoa wa Kilimanjaro unakusudia kutumia huduma za Wakala kutoza ada za maegesho ya vyombo vya usafiri katika maeneo ya hifadhi 2a barabara zote zilizo chini ya usimamizi wake katika Halmashauri ya Manispaa ya Moshi

2. Wakala wa Barabara za vijijini na mjini Tanzania (TARURA) unapenda kuwakaribisha waombaji wenye sifa kutuma maombi yao kwa ajili ya zabuni ya Wakala wa Kutoza Ada za Maegesho ya Vyombo vya Usafiri Kwenye Hifadhi za Barabara Katika Halmashauri ya Manispaa ya Moshi, Zabuni Namba AE/092/2019/2020/KLI/NC/01

3. SIFA ZA MUOMBAJI: Muombaji atatakiwa kuwa na sifa zifuatazo

  • Awe Mtanzania
  • Muombaji awe na mtaji usiopungua Shilingi Milioni Hamsini (TZS. 50.000.000.00).
  • Muombaji awe na ofisi ya kudumu anapofanyia kazi zake.
  • Muombaji awe na leseni hai ya biashara ya uwakala wa utozaji wa ada ya maegesho.
  • Muombaji awe na uzoefu usiopungua miaka miwili kuanzia mwaka 2014 kwenye kazi ya uwakala wa utozaji wa ada ya maegesho ya Vyombo vya Usafiri kwa niaba ya Mamlaka za Serikali za Mitaa hususani Majiji, Manispaa au Taasisi za Serikali.
  • Muombaji awe na cheti cha Utambulisho wa Mlipa kodi (TIN)
  • Muombaji awe na hati halali ya kuthibitisha ulipaji wa kodi (Tax Clearance)
  • Muombaji awe na taarifa za kifedha zilizokaguliwa (Audited Financial Statement) kwa kipindi cha miaka miwili kuanzia 2016 hadi 2018.
  • Muombaji awe na taarifa za kifedha ya benki (Bank Statement) ya kipindi cha kuanzia tarehe 1 Julai, 2018 mpaka tarehe 30 Juni, 2019 yenye mauzo (turnover) yasiyopungua Shilingi Milioni Kuni (10,000,000.00) Taarifa hiyo iwe na “Certificate of Balance” kutoka katika Benki husika.
  • Muombaji awe na cheti cha OSHA kinachoonyesha kukidhi matakwa ya Sheria Na. 5 ya Mwaka 2003
  • Muombaji awe amesajiliwa kwenye Mfuko wa Fidia kwa wafanyakazi (WCF) kwa mujibu wa Sheria ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi Sura ya 263 pitio la Mwaka 2015.
  • Awasilishe taarifa za mashauri ya mahakama (Litigation records).

4. Zabuni zitashughulikiwa kwa utaratibu wa ushindani wa kitaifa [National Competitive Bidding] ulioainishwa kwenye Kanuni za Ununuzi wa Umma za Mwaka 2013, zikisomwa pamoja na marekebisho yake ya Mwaka 2016 na ziko wazi kwa waombaji wote wa hapa nchini.

5. Waombaji wote wenye nia na uwezo wanaweza kupata taarifa kamili kupima makabrasha ya zabuni katika ofisi ya Katibu wa Bodi Kasimu ya Zabuni TARURA Mkoa wa Kilimanjaro, kupitia anuani iliyotajwa kwenye jedwali hapo juu kila siku kuanzia saa mbili kamili (02.00) asubuhi hadi saa tisa na nusu (09:30) kamili alasiri, siku za Jumatatu hadi ljumaa [isipokuwa siku za sikukuu zinazotambulika kitaifa].

6. Muombaji atatakiwa kujaza kwa usahihi na kuwasilisha Fomu ya dhamana ya zabuni (Bid Securing Declaration) kwa muundo unaopatikana kwenye kabrasha la zabuni.

7. Nyaraka 2a Zabuni zitapatikana baada ya kulipa ada stahiki ya zabuni ya Shillingi Laki moja tu (TZS 100,000.00) Kupitia Control Number itakayotolewa na ofisi ya Mratibu wa TARURA Kilimanjaro. Mzabuni atapewa Control Number baada ya kuwasilisha barua ya maombi ya ununuzi wa zabuni. Fedha zitaingizwa kwenye akaunti namba 53010001080 iliyopo katika Benki ya NMB, TARURA Collection Account tawi Ia Kambarage Dodoma. Muombaji atatakiwa kuwasilisha nakala halisi ya hati ya malipo ya Benki ikiambatana na barua ya maombi ya Zabuni husika. Malipo yaliyotolewa kama ada ya maombi ya zabuni hayatarejeshwa.

8. Zabuni zote ziwe na nakala halisi (original) moja (1) na nakala (copies) tatu (3) zinazofanana zifungwe ndani ya bahasha iliyofungwa kwa Iakiri na juu ya bahasha ziandikwe maelezo ya Zabuni na kisha iandikwe na kuwasilishwa kwa anuani ifuatayo: Katibu wa Bodi Kasimu ya Zabuni TARURA Mkoa wa Kilimanjaro, S. L. P. 7425, Moshi, (Jengo la NSSF mkabala na ofisi za Manispaa ya Moshi, ghorofa ya pili)

9. Siku ya mwisho ya kuwasilisha maombi ya zabuni ni tarehe 23 Agosti, 2019 kabla ya saa 05:30 asubuhi. Zabuni zitafunguliwa hadharani mara tu baada ya muda wa mwisho wa kuwasilisha zabuni. waombaji wote au wawakilishi wao wanaalikwa kuhudhuria ufunguzi wa zabuni hizo utakao fanyika siku hiyo katika ofisi ya Mratibu wa TARURA Mkoa wa Kilimanjaro

10. Wakala wa Barabara za Vuumi na Mijini Tanzania (TARURA) hautalazimika kukubali/ kutokukubali kutoa zabuni kwa mwombaji yeyote kutokana na kigezo cha malipo makubwa/malipo kidogo ya zabuni.

11. Zabuni zitakazochelewa kuwasilishwa, zabuni za kielektroniki. na zabuni zisizofunguliwa katika tukio la ufunguaji zabuni. kwa hali yoyote ile hazitakubaliwa kwa tathmini.

Eng. Meleck Y. Silaa
MRATIBU WA MKOA
WAKALA WA BARABARA ZA VIJIJINI NA MIJINI
TANZANIA (TARURA)

Source; Mwananchi

WhatsApp
Twitter
Email
LinkedIn
Instagram

Related