TARURA

Tangazo la Zabuni ya Wakala wa Utozaji wa Ada za Maegesho ya Vyombo vya Usafiri Kwenye Hifadhi Za Barabara za Halmashauri ya Manispaa ya Singida Mjini, Ikungi, Singida Vijijini, Manyoni, na Iramba Mkoa Wa Singida

WhatsApp
Twitter
Email
LinkedIn
Instagram

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA -WAKALA WA BARABARA ZA VIJIJINI NA MIJINI (TARURA)

TANGAZO LA ZABUNI

SINGIDA ZABUNI NA AE/092/2018/2019/SGD/NC/1 YA

WAKALA WA UTOZAJI WA ADA ZA MAEGESHO YA VYOMBO VYA USAFIRI KWENYE HIFADHI ZA BARABARA ZA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA MJINI, IKUNGI, SINGIDA VIJIJINI, MANYONI, NA IRAMBA MKOA WA SINGIDA

Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini Tanzania (TARURA) Mkoa wa Smgida unakusudia kutumia huduma za Wakala kutoza ada za maegesho ya vyombo vya usafiri katika maeneo ya hifadhi za barabara zote zillzo chini ya usimamizi wake katika Halmashauri ya Singida Mjini. lkungi Singida Vu‘ljini, Manyoni, na Iramba.

Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini Tanzania (TARURA) unapenda kuwakaribisha waombaji wenye sifa kutuma maombi yao kwa ajili ya zabuni ya Wakala wa Kutoza Ada za Maegesho ya Vyombo vya Usafiri Kwenye Hifadhi za Barabara Katika Halmashauri ya Singida Mjini, Ikungi, Singida Vijijini, Manyoni na Iramba Zabuni Namba AE/092/2018/2019/SGD/NC/1

SIFA ZA MUOMBAJI: Muombaji atatakiwa kuwa na sifa zifuatazo:

  1. Awe Mtanzania
  2. Muombaji awe ni Kampuni iliyosajlliwa kwa mujibu wa Sheria za Tanzania na ambayo haijawahi kuzuiwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) kujihusisha na shughuli za Ununuzi wa Umma.

iii. Muombaji awe na mtaji usiopungua Shilingi Mllioni Hamsini ambao umeainishwa kwenye Memoranda ya Kampuni (Memorandum and Articles of Association) au ushahidi kuwa kampuni iliongeza mtaji wake.

  1. Muombaji awe na ofisi ya kudumu anapofanyia kazi zake.
  2. Muombaji awe na leseni hai ya biashara ya uwakala wa utozaji wa ada ya maegesho.
  3. Muombaji awe na uzoefu usiopungua miaka miwili kuanzia mwaka 2014 kwenye kazi ya uwakala wa utozaji wa ada ya maegesho ya Vyombo vya Usaflri kwa niaba ya Mamlaka za Serikali za Mitaa hususani MajiJi, Manispaa au Taasisi za Senkali.

vii. Muombaji awe na cheti cha Utambulisho wa Mlipa kodi (TIN)

viii. Muombaji awe amesajiliwa kulipa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT)

  1. Muombaji awe na hati halali ya kuthibitisha ulipaji wa kodi (Tax Clearance)
  2. Muombaji awe na taan’fa za kifedha zilizokaguliwa (Audited Financial Statement) kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia 2016 hadi 30 June 2018 yenye mauzo (turnover) yasiyopungua Shilingi Milioni Mia (100.000.000.00).
  3. Muombaji awe na cheti cha OSHA kinachoonyesha kukidhi matakwa ya Shena Na. 5 ya Mwaka 2003

xii. Muombaji awe amesajiliwa kwenye Mfuko wa Fidia kwa wafanyakazi (WCF) kwa mujibu wa Sheria ya Mfuko wa Fldla kwa Wafanyakazi Sura ya 263 pitio 1a Mwaka 2015.

xiii. Muombaji awe na sifa njema ya kufanya kazi ya Uwakala wa kukusanya ada za maegesho ya vyombo vya usafiri kwa niaba ya Mamlaka za Serlkali za Mitaa hususani Manispaa na Majiji, au Taasisi za Serikali.

xiv. Asiyewahi kukutwa na hatia baada ya Mashauri katika chombo chochote cha Kisheria kuhusiana na mkataba wa aina yoyote na Taasisi yoyote ya Serikali.

Zabuni zitashughulikiwa kwa utaratibu wa ushindani wa kitaifa National Competitive Bidding] ulioainishwa kwenye Kanuni za Ununuzi wa Umma za Mwaka 2013, zikisomwa pamoja na marekebisho yake ya Mwaka 2016 na ziko wazi kwa waombaji wbte wa hapa nchini.

Waombaji wote wenye nia na uwezo wanaweza kupata taarifa kamili kupitia makabrasha ya zabuni katika ofisi ya Katibu wa Bodi Kasimu ya Zabuni TARURA Mkoa wa Singida kupitia anuani iliyotajwa kwenye jedwali hapo juu kila siku kuanzia saa mbili kamili (02.00) asubuhi hadi saa tisa (09:30) na nusu alasiri, snku za Jumatatu hadi Ijumaa [Isipokuwa siku za sikukuu zinazotambuhka kitaifa].

Muombaji atatakiwa kuiaza kwa usahihi na kuwasilisha Fomu ya dhamana ya zabuni Bid Securing Declaration kwa muundo unayopatikana kwenye kabrasha la zabuni.

Nyaraka za Zabuni zitapatikana baada ya kulipa ada stahiki ya zabuni ya Shilingi Laki moja tu (100,000.00) Kupstia akaunti namba 53010001080 iliyopo katika Benki ya NMB. TARURA Collection Account Muombaji atatakiwa kuwasilisha nakala halisi ya hati ya malipo ya Benki ikiambatana na barua ya maombi ya Zabuni husika. Malipo yaliyotolewa kama ada ya maombi ya zabuni hayatarejeshwa.

Zabuni zote ziwe na nakala halisi (origina1) moja (1) na nakala (copies) tatu (3) zinazofanana zifungwe ndani ya bahasha iliyofungwa kwa lakiri najuu ya bahasha ziandikwe maelezo ya Zabuni na kisha iandikwe na kuwasilishwa kwa anuani ifuatayo: Katibu wa Bodi Kasimu ya Zabuni TARURA Mkoa wa Singida S. L. P. 539 Singida, Singidani Complex ghorofa ya tatu.

Siku ya mwisho ya kuwasilisha maombi ya zabuni ni tarehe 3/6/2019 kabla ya saa 05:30 asubuhi. Zabuni zitafunguliwa hadharani mara tu baada ya muda wa mwisho wa kuwasilisha zabuni, waombaji wote au wawakilishi wao wanaalikwa kuhudhuria ufunguzi wa zabuni hizo utakao fanyika siku hiyo katika ofisi ya Mratibu wa TARURA Mkoa wa Singida.

Wakala wa Barabara za Vijijini na Mljini Tanzania (TARURA) hautalazimika kukubali/ kutokukubali kutoa zabuni kwa mwombaji yeyote kutokana na kigezo cha malipo makubwa/malipo kidogo ya zabuni.

Zabuni zitakazochelewa kuwasilishwa, zabuni za kielektroniki. na zabuni zisizofunguliwa katika tukio Ia ufunguaji zabuni, kwa hali yoyote ile hazitakubaliwa kwa tathmini.

MRATIBU MKOA WA SINGIDA
WAKALA WA BARABARA ZA VIJIJINI NA MIJINI TANZANIA (TARURA)
Source; Mwananchi
Date; 20/05/2019

WhatsApp
Twitter
Email
LinkedIn
Instagram

Related