TARURA

Tangazo la Zabuni ya Wakala wa Utozaji wa Ada za Megesho ya Vyombo vya Usafiri Kwenye Hifadhi za Barabara za Halmashauri ya Manispaa Mtwara Mikindani

WhatsApp
Twitter
Email
LinkedIn
Instagram

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

WAKALA WA BARABARA ZA VIJIJINI NA MIJINI (TARURA)

TANGAZO LA ZABUNI

ZABUNI NA AE/092/2019-2020/MT/NC/09

WAKALA WA UTOZAJI WA ADA ZA MAEGESHO YA VYOMBO VYA USFIRI KWENYE HIFADHI ZA BARABARA ZA HALMASHAURI YA MANISAPAA MTWARA MIKINDANI

I. Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini Tanzania (TARURA) Mkoa wa MTWARA unakusudia kutumia huduma za Wakala kutoza ada za maegesho ya vyombo vya usafiri katika maeneo ya hifadhi za barabara zote zilizo chini ya usimamizi wake katika Halmashauri ya Manispaa Mtwara Mikindani.

2. Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini Tanzania (TARURA) unapenda kuwakaribisha waombaji wenye sifa kutuma maombi yao kwa ajili ya zabuni Na. AE/092/2019-2020/MT/NC/09 ya Wakala wa Kutoza A,da za Maegesho ya Vyombo vya Usafiri Kwenye Hifadhi za Barabara Katika
Halmashauri ya Manispaa Mtwara Mikindani

SIFA ZA MUOMBAJI: Muombaji atatakiwa kuwa na sifa zifuatazo
i. Awe Mtanzania
ii. Muombaji awe ni Kampuni iliyosajiliwa kwa mujibu wa Sheria za Tanzania na ambayo haijawahi kuzuiwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) kujihusisha na shughuli za Ununuzi wa Umma.
iii. Muombaji awe na mtaji usiopungua Shilingi Milioni Kumi (10, 000,000.00) ambao umeainishwa kwenye Memoranda ya Kampuni (Memorandum and Articles of Association) au ushahidi kuwa kampuni iliongeza mtaji wake na awasilishe hati fungani ya benki yenye thamani ya shilingi milioni kumi (10,000,000.00).
iv. Muombaji awe na ofisi ya kudumu anapofanyia kazi zake.
v. Muombaji awe na leseni hai ya biashara ya uwakala wa utozaji wa ada ya maegesho.
vi. Muombaji awe na uzoefu usiopungua miaka miwili kuanzia mwaka 2014 kwenye kazi ya uwakala wa utozaji wa ada ya maegesho ya Vyombo vya Usafiri kwa niaba ya Mamlaka za Serikali za Mitaa hususani Majiji. Manispaa au Taasisi za Serikali.
vii. Muombaji awe na cheti cha Utambulisho wa Mlipa Kodi (TIN)
viii. Muombaji awe amesajiliwa kulipa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT)
ix. Muombaji awe na hati halali ya kuthibitisha ulipaji wa kodi (Tax Clearance)
x. Muombaji awe na taarifa za kifedha zilizokaguliwa (Audited Financial Statement) kwa kipindi cha miaka miwili kuanzia 2016 hadi 2018.
xi. Muombaji awe na taarifa za kifedha ya benki (Bank Statement) ya kipindi cha kuanzia tarehe I Januari . 2018 mpaka tarehe 30 Mei. 2019 yenye mauzo (turnover) yasiyopungua Shilingi 30,000,000.00 Taarifa hiyo iwe na “Certificate of Balance” kutoka katika Benki husika.
xii. Muombaji awe na sifa njema ya kufanya kazi ya Uwakala wa kukusanya ada za maegesho ya vyombo vya usafiri kwa niaba ya Mamlaka za Serikali za Mitaa hususani Manispaa , Majiji au Taasisi za Serikali.
xiii. Asiyewahi kuwa na mashauri katika chombo chochote cha Kisheria kuhusiana na mkataba wa aina yoyote na Taasisi yoyote ya Serikali.

4. Zabuni zitashughulikiwa kwa utaratibu wa ushindani wa kitaifa [National Competitive Bidding] ulioainishwa kwenye Kanuni za Ununuzi wa Umma za Mwaka 2013, zikisomwa pamoja na marekebisho yake ya Mwaka 2016 na ziko wazi kwa waombaji wote wa hapa nchini.

5. Waombaji wote wenye nia na uwezo wanaweza kupata taarifa kamili kupitia makabrasha ya zabuni katika ofisi ya Katibu wa Bodi kasimiwa ya Zabuni TARURA Mkoa wa MTWARA, kupitia anuani iliyotajwa kwenye jedwali hapo juu kila siku kuanzia saa mbili kamili (02.00) asubuhi hadi saa tisa (09:00) kamili alasiri. siku za Jumatatu hadi Ijumaa [isipokuwa siku za sikukuu zinazotambulika kitaifa].

6. Muombaji atatakiwa kujaza kwa usahihi na kuwasilisha Fomu ya dhamana ya zabuni Bid securing Declaration kwa muundo unaopatikana kwenye kabrasha la zabuni.

7. Nyaraka za Zabuni zitapatikana baada ya kulipa ada stahiki ya zabuni ya Shillingi za Tanzania Laki Moja tu (TZS 100,000.00) Kupitia akaunti namba 53010001080 iliyopo katika Benki ya NMB, inayotambulika kwa jina la TARURA Collection Account. Muombaji atatakiwa kuwasilisha nakala halisi ya hati ya malipo ya Benki ikiambatana na barua ya maombi ya Zabuni husika. Malipo yaliyotolewa karna ada ya maombi ya zabuni hayatarejeshwa. Malipo haya yafanyike baada ya kupata “control” namba. Kwa mawasiliano kuhusu “control” namba piga 0625770979

8. Zabuni zote ziwe na nakala halisi (original) moja (I) na nakala (copies) tatu (3) zinazofanana zifungwe ndani ya bahasha iliyofungwa kwa lakiri na juu ya bahasha ziandikwe maelezo ya Zabuni unayoomba na kisha kuwasilishwa kwa anuani ifuatayo: Katibu wa Bodi Kasimu ya Zabuni TAR URA Mkoa_wa Mtwara S. L. P .,1443, MTW ARA.

9. Siku ya mwisho ya kuwasilisha maombi ya zabuni ni tarehe_()5.08. 2019 kabla ya saa 10;00 asubuhi. Zabuni zitafunguliwa hadharani mara tu baada ya muda wa mwisho wa kuwasilisha zabuni , waombaji wote au wawakilishi wao wanaalikwa kuhudhuria ufunguzi wa zabuni hizo utakao fanyika siku hiyo katika ofisi ya Mratibu wa TARURA Mkoa wa Mtwara iliyopo jengo la Ushirika wa Wakulima mkabala na Ofisi za Posta Mkoa Mtwara.

10. Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini Tanzania (TARURA) hautalazimika kukubali/ kutokukubali kutoa zabuni kwa mwombaji yeyote kutokana na kigezo cha malipo makubwalmalipo kidogo ya zabuni.

11. Zabuni zitakazochelewa kuwasilishwa , zabuni za kielektroniki, na zabuni zisizofunguliwa katika tukio la ufunguaji wa zabuni, kwa hali yoyote ile hazitakubaliwa kwa tathmini.

Mratibu wa Mkoa wa Mtwara kwa niaba ya
Mtendaji Mkuu
Wakala wa barabara za Vijijini na Mijini Tanzania (TARURA)

WhatsApp
Twitter
Email
LinkedIn
Instagram

Related