TFC

TANGAZO LA ZABUNI

WhatsApp
Twitter
Email
LinkedIn
Instagram

Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania (TFC) kushirikiana na wadau wa mradi wa Ushirika
wametenga kiasi cha fedha kwa ajili ya kugharamia zabuni za kuendesha majengo ya Ushirika
yaliyopo Kitalu 76/77 Mtaa wa Lumumba llala Dar Es Salaam kwa mwaka wa fedha 2023/2024.

Shirikisho linatoa Tangazo la zabuni za watoa huduma mbalimbali katika majengo ya Ushirika
Mtaa wa Lumumba kama zilivyoorodheshwa hapo chini.

Tangazo hili la zabuni liko wazi kwa kampuni na taasisi yoyote iliyosajiliwa kisheria kutoa
huduma husika na Nyaraka ya zabuni itapatikana Ofisi za Shirikisho la Vyama vya Ushirika
Tanzania (TFC) baada ya kulipia ada ya zabuni iliyotajwa ambayo haitarejeshwa kiasi cha TZS
200,000/= ambazo zitalipwa kwa akaunti namba: 01J1007451700 Benki: CRDB, Jina la akaunti:
Tanzania Federation of Cooperatives Ltd.

Maombi ya zabuni yazingatiwe masharti yafuatayo:-

  1. Mwombaji awe ni kampuni iliyo sajiliwa kwa mujibu wa sheria na aandike barua ya maombi.
  2. Fomu ya maombi ya zabuni ijazwe na kusainiwa na wenye haki halali wa kisheria (power
    attorney) katika zabuni husika.
  3. Mwombaji atatakiwa aambatanishe;- a) Kivuli cha leseni ya biashara ilio hai anayo kusudia kutumia katika zabuni b) Kivuli cha usajili wa kampuni c) Cheti cha usajili wa TIN/VAT na Kifaa cha kutolea risiti za malipo ya fedha cha Elekroniki (EFD devices) d) Fomu ya zabuni ikiwa imejazwa kikamilifu na kusainiwa Aidha nyaraka zote ziwe zimethibitishwa na mwanasheria (certified true copy of original)
  1. Pamoja na matakwa yaliorodheshwa hapo juu:-
    a) Waorodheshe kazi alizokwisha fanya na anazoendelea kufanya kwa kipindi cha miaka 3 iliyopita
    na thamani ya kazi husika.
    b) Idadi ya Watumishi katika kampuni yake na sifa walizonazo
    c) Vibali vya ruhusa ya kufanya kazi husika kutoka mamlaka za serikali.
    d) Mzabuni ni lazima ainishe bayana ilipo Ofisi yake ikiwemo namba ya kitalu
  2. Mwombaji yoyote atakayeshindwa masharti yaliyo orodheshwa ya zabuni atakuwa amejiondoa mwenyewe katika ushindani.
  3. Mwombaji atapaswa kuweka dhamana ya utekelezaji wa mkataba (Performance Bond ikiwa ni
    Banker’s Guarantee) kwa kiwango cha 2% (asilimia mbili) ya bei ya mkataba.
  4. Mwombaji awe tayari kuambatanisha fomu ya Usalama wa zabuni/Tender Security declaration
    25%.
  5. Mwombaji awe tayari kupokea malipo yake baada ya kazi kufanyika na kutoa ankra ya madai ili kupokea malipo kupitia akaunti yenye jina la kampuni.
  6. Kabrasha za zabuni zinapatikana katika Ofisi ya Katibu Mtendaji, Shirikisho la Vyama vya
    Ushirika Tanzania (TFC), S.L.P 2567, DAR ES SALAAM ghorofa ya kumi na sita(16) Kuanzia
    saa tatu (3) asubuhi hadi saa kumi(10) kamili Jioni siku za kazi, kuanzia Jumatatu hadi ljumaa.
  7. Maombi ya zabuni yenye Lakili na kubainisha namba ya zabuni yatumwe kupitia Ofisi ya
    katibu Mtendaji Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania (TFC) kwa anwani iliyo orodheshwa
    hapo chini kabla ya tarehe 07/06/2023 saa 4.00 kamili asubuhi.
  8. Zabuni zote zitafunguliwa mbele ya wazabuni au wawakilishi wao tarehe 07/06/2023 saa 4.00
    kamili asubuhi
  9. Zabuni zitakazochelewa kufika, kutokufika au kutumwa kwa njia ya elektroniki
    hazitafunguliwa, aidha Zabuni zitakazo tumwa kwa njia ya posta zitumwe mapema kwa rejister.

Katibu Mtendaji
Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania (TFC),
S.L.P 2567,
DARES SALAAM.
17 Mei 2023

WhatsApp
Twitter
Email
LinkedIn
Instagram

Related