utumishi

Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa-TAMISEMI

WhatsApp
Twitter
Email
LinkedIn
Instagram

Madhumuni ya kuwepo kwa Serikali za Mitaa ni kupeleka  Madaraka kwa Wananchi ambapo chimbuko lake ni Katiba ya Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 katika Sura ya 8, Ibara ya 145 na  146. Upelekeaji wa madaraka kwa wananchi unapitia katika Mamlaka za  Serikali za Mitaa na ndiyo maana Serikali za Mitaa na ushirikishwaji wa  Wananchi katika mchakato wa maendeleo vimetambuliwa katika Katiba na  Sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Wakati Nchi yetu inapata  uhuru wake kulikuwa na majimbo kumi ya Utawala ambayo yaliritihiwa toka  utawala wa kikoloni wa Kiingereza mwaka 1966. Rais wa kwanza Hayati  Julius Kambarage Nyerere kwa Mamlaka aliyopewa aliunda Mikoa 15 na  kuondoa utaratibu wa mgawanyo wa nchi katika Majimbo. Hadi Sasa Nchi  yetu ina Mikoa 26, Wilaya 139, Halmashauri 184, Tarafa 570, Kata 3,956,  Vijiji 12,319, Vitongoji 64,384 pamoja na Mitaa 4,263. Baada ya uhuru  Halmashauri zilikuwa jumla 45 na hadi kufikia mwaka 2009 zilikuwa  Halmashauri 129 na zimeendelea kuongezeka hadi kufikia 184 mwaka 2021.

Wakati  wa Uhuru hakukuwa na Halmashauri za Majiji na sasa kuna Halmashauri za  Majiji 6, kulikuwa na Halmashauri ya Manispaa moja ya Dares Salaam na  sasa kuna Halmashauri za Manispaa 20, Halmashauri za Miji zilikuwa 9 na  sasa Halmashauri za Miji ni 21 na Halmashauri za Wilaya zilikuwa 10 na  sasa zipo Halmashauri za Wilaya 137.

Majukumu ya Ofisi ya Rais – TAMISEMI

Majukumu ya OR-TAMISEMI yanatekelezwa katika ngazi ya Makao Makuu, Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa. Kwa kuzingatia Hati ya Rais ya Mgawanyo wa Majukumu (Presidential Instrument) iliyotolewa na Rais  Aprili 2016, majukumu ya OR-TAMISEMI ni pamoja na:-

i)    Kuratibu utekelezaji wa Sera ya  Maendeleo  Mijini na Vijijini  na Upelekaji wa Madaraka kwa Umma (D by D);

ii)    Kuratibu huduma mijini kama vile usafirishaji, maji na usafi wa mazingira;

iii)    Kusimamia Tume ya Utumishi wa Walimu;

iv)    Kuratibu na Kusimamia Tawala za Mikoa ili ziweze kuziwezesha Halmashauri  kutekeleza wajibu wake;

v)    Kuratibu Usimamizi na Uendeshaji wa Shule za Msingi na Sekondari nchini kupitia Mamlaka za Serikali za Mitaa (MSM);

vi)    Kujenga uwezo wa watumishi wa OR-TAMISEMI ili watekeleze majukumu yao kwa ufanisi; na

vii)    Kusimamia utendaji wa Mashirika, Taasisi, Programu na miradi iliyo chini ya OR-TAMISEMI

FOR MORE INFORMATION CLICK HERE OFFICIAL WEBSITE FOR TAMISEMI

WhatsApp
Twitter
Email
LinkedIn
Instagram

Related