Crude Oil Pipeline-EACOP

UTOAJI WA HUDUMA ZA UKARABATI KATIKA JENGO LA OFISI ZA MAKAO MAKUU YA EACOP

WhatsApp
Twitter
Email
LinkedIn
Instagram

MAOMBI YA KUONESHA NIA YA UTOAJI WA
HUDUMA ZA UKARABATI KATIKA JENGO LA
OFISI ZA MAKAO MAKUU YA EACOP
KUMBUKUMBU NA. 00000234
Kampuni ya Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) Ltd, (“EACOP LTD”) inaalika
kampuni yenye uzoefu na weledi wa kutosha kuonesha nia ya kutoa huduma za ukarabati katika
jengo la ofisi za makao makuu ya Mradi wa EACOP
Mradi wa EACOP unajumuisha shughuli za ujenzi na uendeshaji wa bomba la kusafirisha Mafuta
lililofukiwa chini ya ardhi linalokatisha mipaka ya nchi mbili kwa ajili ya kusafirisha Mafuta katika
masoko ya kimataifa. Bomba litaanzia Kabaale katika Wilaya ya Hoima, nchini Uganda, mpaka
rasi ya Chongoleani, karibu na Mkoa wa Tanga, nchini Tanzania. Urefu wa bomba ni kilomita
1,443, kati yake kilomita 1,147 zitakuwa nchini Tanzania
MAELEZO MAFUPI KUHUSU HUDUMA
Kampuni EACOP Ltd, inatumia sehemu ya ghorofa nne zenye jumla ya mita za mraba [***] katika
Jengo lililopo Kitalu 1, Kiwanja Na. 1403 nyumba Na. 7, Mtaa wa Bains Avenue, Off Chole, Dar
es Salaam. Kama sehemu ya matengenezo na utunzaji wa maeneo yanayotumiwa na ofisi zake,
Kampuni ya EACOP Ltd inahitaji huduma ya mtu/makampuni yenye sifa kutoa huduma zifuatazo;

  • Kufanya ukarabati na/ama wa mara kwa mara au wa kulinda mfumo wa HVAC.
  • Kufanya ukarabati na/ama wa mara kwa mara au wa kulinda mifumo ya maji ya jengo, (ikiwa ni
    pamoja na kubadilisha machujio, vifuniko, gasiketi, n.k)
  • Kufanya ukarabati na /ama wa mara kwa mara au wa kulinda seti ya mfumo wa jenereta kwenye
    jengo ikiwa ni pamoja na (ATS, elementi za chujio, Kubadilisha Mafuta nk)
  • Kupigiwa simu kwa ajili ya usaidizi wa kazi za matengenezo ya dharula (Kazi za Umeme, Mfumo
    wa Usafi (ikujumuisha matengenezo ya mabomba yanayohusiana na pampu ya jengo, kudhibiti
    uvujaji kutoka kwenye mabomba na valvu, Miundo mbinu ya usafi, miundo mbinu ya usambazaji
    wa maji n.k), Mifumo ya AC (kama ipo).
  • Kupigiwa simu kwa jili ya Kazi za matengenezo madogo / ya kati ya (Mitambo / Umeme).
  • Kuzibua mambomba ya mifumo ya maji na maji taka, maunganio ya mabomba na vifuniko vya
    kalo. Usambazaji wa maji, Mashimo ya maji taka & kazi ya Uteketezaji Maji taka
    Kumbuka: Orodha ni kielelezo tu na sio kamili kabisa. Wigo wa kazi na huduma
    utakamilishwa baada ya EOI na utajumuishwa katika CFT itakayotolewa baadae.
    VIGEZO MUHIMU:

Makampuni au taasisi zinzoonesha nia zinakaribishwa kutuma maombi na kuambatanisha
nyaraka zifuatazo.

  • Cheti halali cha kampuni na leseni ya biashara
  • Cheti cha namba ya utamburisho wa mlipa kodi pamoja na cheti cha TRA cha uthibitisho wa kulipa
    kodi kwa mwaka wa fedha uliopita
  • Waombaji wanasisitizwa sana kuhakikisha kuwa wamejisajili au wametuma maombi ya kujisajili
    kwenye kazi data ya EWURA (LSSP) ya Watoa Huduma za Ugavi wa Ndani, wakati wa
    kuwasilisha maombi ya kuonesha nia,
  • Usajili wa mamlaka husika wa hivi karibuni ikijumuisha OSHA, CRB, etc
  • Kuzingatia Kanuni za Watoa Huduma wa Ndani za mwaka 2017 Uzoefu wa awali wa kutoa
    Huduma zinazofanana na huduma za Ukarabati kwa kipindi cha miaka 5 iliyopita.
  • Provide proof of financial capacity and financial statement for the previous financial year
  • Uthibitisho uwezo wa kifedha na taarifa ya kifedha ya mwaka wa fedha uliopita
  • Upatikanaji wa rasilimali za Kiufundi (Lazima kuambatanisha na sifa bainifu (CV) na uzoefu wa
    miaka ya kutoa huduma
  • Barua ya uthibitisho kuhusu usimamizi wa miundo mbinu na ukarabati wa vitu katika mawanda
    unganifu yanajuumuisha Ukarabati na Matengenezo ya Ofisi kutoka kwa miradi iliyotekelezwa
    hapo awali katika kipindi cha miaka 5 iliyopita kama vile miradi ya (Bomba, Umeme, Ukarabati wa
    vyoyozi, Ufundi seremala, Upakaji rangi, Ufundi washi).
    Makampuni yenye uwezo na rasilimali za kutosha kutekeleza shughuli zilizotajwa hapo juu
    yanakaribishwa kutuma maombi pamoja na kuambatanisha nyaraka zilizotajwa hapo juu kupitia
    barua pepe ya [email protected] , (ukubwa wa barua pepe usizidi 20Mb).
    Maombi yatumwe mnamo au kabla ya tarehe 11 Juni 2023 saa 11 jioni saa za Afrika
    Mashariki. Kichwa cha Barua pepe kiwe 00000234 – Utoaji wa huduma ya Matengenezo na
    Ukarabati Mkubwa katika Mradi wa EACOP Maombi yote ya kuonesha nia (EOI) yawe kati ya
    kurasa 10 hadi 20. Maombi yote lazima yaandikwe kwa lugha ya Kingereza
    Muhimu: Kampuni ya EACOP LTD itapitia na kuchambua nyaraka zilizotumwa na makampuni
    yenye nia kulingana na EOI hii na kisha kufanya tathmini kwa kutumia vigezo vya ndani ili
    kubaini makampuni yatakayojumuishwa kwenye orodha ya (Makampuni) ya awali yaliyokidhi
    vigezo. Makampuni yaliyofuzu hatua za awali pekee ndiyo yatakayopewa mwaliko wa zabuni,
    kwa kutia saini Mkataba wa Kutunza Siri (NDA), kama mwendelezo wa wito wa mchakato wa
    utoaji wa zabuni. Kampuni ya EACOP LTD inayo haki ya kufanya maamuzi yake ya kuchagua
    au kukataa kampuni na kuheshimu maamuzi yake pasipo kutoa sababu kwa kampuni husika.
WhatsApp
Twitter
Email
LinkedIn
Instagram

Related