tfs

UUZAJI WA MAGOGO YA MTI AINA YA MKURUNGU KWA NJIA YA MNADA KATIKA KIJIJ CHA WACHAWASEME (IGAGALA No 9) NA KIJIJI CHA MPWAGA (IGAGALA No 3) WILAYANI KULIUA MKOA WA TABORA

WhatsApp
Twitter
Email
LinkedIn
Instagram

UUZAJI WA MAGOGO YA MTI AINA YA MKURUNGU KWA NJIA YA MNADA KATIKA KIJIJ CHA WACHAWASEME (IGAGALA No 9) NA KIJIJI CHA MPWAGA (IGAGALA No 3) WILAYANI KULIUA MKOA WA TABORA

  • Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) utauza magago ya Mkurungu (Pterocarpus tinctorius) jumla ya vipande 7,456 vye jumla ya meta za ujazo 1,758.793. Magogo hayo yapo katika kijij cha Wachawaseme na Mpwaga , Tarafa ya Igagala, Wilaya ya Kaliua , Mkoani Tabora.
  • Magogo hayo ya Mkurungu yamepimwa na yamepangwa katika mafunguu (lots) 10 na yatauzwa kwa njia ya mnada wa hadhara kwa kuzingatia Kanuni ya 31 (iii) ya Kanuni za Sheria ya Misitu za Mwaka 2004. Magogo hayo yatauzwa nahali yalipohifadhiwa na jinsi yalivyo na mnunuzi hatakuwa na haki ya kudai fidia baada ya mauzo.
  • Mnada utafanyika hadharani katika vijij vya Wachawaseme na Mpwaga wakiwepo wanunuzi wote.Mnada utafanyika  siku ya jumatatu ya tarehe 20 september ,2021 kuazia saa 4:39 asubuhi.
  • Mnunuzi anakaribishwa kutembelea Kijij cha Wachawaseme na Mpwaga kilipopangwa mafungu (lots) ya Magogo ya Mkurungu ili kukangua hayo ya misitu muda wa kazi kuazia saa (03:00)asubuhi alasiri siku za Jumatatu hadi Ijumaa. Ukaguzi huo utafanyika kuazia tarehe ya Tangazo hili hadi Tarehe 19/09/2021.Aidha, maafisa Misitu wa WAKALA (TFS) watakuwepo kwa ajiri ya kutoa maelezo ya ziada ikiwa yatahitajika . Jedwali hili litatumika kuchangua fungu lenye magogo ya kununua kwa kuzingatia taarifa zilizoorodheshwa kama ifuatavya:
  • Mnunuzi atakayeshida atatakiwa kulipa asilimia 25% ya thamani yote ya ununuzi siku ya mnada . Fedha hizo hazitarudishwa endepo mshindi atashindwa kulipia ujazo wote aliouziwa . Aidha , asilimia sabini na tano (75%) iliyobaki atalipwa ndani ya siku kumi na nne (14) kuazia siku ya tarehe ya toleo la barua ya ushindi kwa mnunuzi . Malipo yote yatafanyika kupitia benki au mitandao ya watoa huduma za kifedha baada ya kupewa hati ya madai (bill) kutoka Mfumo wa Makusanyo ya Wizara ya Maliasili na Utalii (mnrt portal) itakayotolewa na Ofisi ya Wakala wa Huduma za Misiti Tanzania (TFS) Kaliua
  • Atakayeshida fungu husika atalazimika kulipia ushuru wa asilimia tano (5%) ya mazao hayo kwa Halmashauri ya wilaya Kaliua.
  • Mnunuzi atayeshida mnada atatakiwa kuondoa mazao ya misitu aliyonunua ndani ya siku kumi na nne (14) baada ya kumaliza kulipa malipo yote kwa asilimia 100. Baada ya tarehe hizo ulinzi wa mazao hayo yatakuwa juu ya mnunuzi mwenyewe.
  • Mnunuzi aliyeshida atapaswa kuwasilisha hati ya malipo (pay -in- slip) kwa Mhifadhi Misiti Wilaya ya Kaliua kama uthibitisho wa malipo na zaindi ya siku tatu (3) baada ya malipo kufanyika
  • Usajiri wa wanunuzi na watazamaji wenye nia ya kushiriki mnada utafanyika katika kijij cha Wachawaseme na Mpwaga kuazia saa moja na nusu (07:30) asubuhi hadi saa nne kamili (10:00) asubuhi siku ya mnada. Aidha, wanunuzi watakaochelewa kuwasilisha nia zao kwa siku na muda uliopangwa hawataruhusiwa kushiriki katika mnada.
  • Aidha, kibali cha kusafirisha magogo nje ya nchi kitatolewa kwa tangazo maalum la serikali (Government Notes) kwa mshindi atakayehitaji kusafirisha magogo hayo ya nchi.
  • Tangazo hill pia linapatikan katika tovuti zifuatazo za:www.tfs.go.tz na www.mnrt.go.tz

Limetolewa na

KAMISHNA WA UHIFADHI

WAKALA WA HUDUMA ZA MISITI TANZANIA

S.L.P 40832

DAR ES SALAAM

WhatsApp
Twitter
Email
LinkedIn
Instagram

Related