6tenda7

WITO WA PILI WA ANDIKO LA KUOMBA UFADHILI

WhatsApp
Twitter
Email
LinkedIn
Instagram

Muhtasari
Programu ya CookFund, inayofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (European Union), ni programu ya
miaka mitatu (2022 – 2024) inayolenga kuharakisha upatikanaji wa nishati safi na vifaa bora vya
kupikia Tanzania Bara, ikilenga mikoa mitano ambayo ni Dar es Salaam, Pwani, Morogoro,
Dodoma na Mwanza. Programu hii inatekelezwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya
Mitaji (UNCDF) kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo ya Viwanda la Umoja wa Mataifa
(UNIDO) na Wizara ya Nishati nchini Tanzania.

Programu hii inatoa msaada wa kifedha na kiufundi kwa madhumuni ya kuchangia juhudi za
Tanzania katika mapambano dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa kwa kuongeza idadi ya watu
wanaotumia nishati bora na endelevu za kupikia, na hatimaye kuboresha mazingira, ajira na fursa
za kibiashara. CookFund inatoa msaada kutokana na matokeo yatakayofikiwa (performance based),
kwa madhumuni ya kutatua changamoto za mitaji kwa wafanyabiashara na pia kutoa unafuu wa bei
kwa watumiaji wa mwisho wa nishati zinazolengwa (gesi ya kupikia, majiko sanifu ya mkaa,
majiko ya umeme ya mvuke, bioethanol na mkaa mbadala).

Wito wa Maandiko ya Kuomba Ufadhili

UNCDF inawakaribisha wafanyabiashara na makampuni yanayojishughulisha na mnyororo wa
thamani wa nishati safi na vifaa/teknolojia bora za kupikia katika maeneo ya mijini ya mikoa ya
mradi, kuandika na kuomba ufadhili wa kiufundi na kifedha kupitia wito huu wa pili katika
Programu ya CookFund. Maombi: Mwongozo, Vigezo na Fomu maalumu ya maombi, zinaweza
kupakuliwa kutoka kwenye tovuti ya mradi, i.e. https://www.uncdf.org/cookfund.

Lugha: Maombi yote yawasilishwe kwa lugha ya Kiingereza.

Mwisho wa kuwasilisha maombi: Raundi ya pili ya maombi itakuwa wazi kuanzia tarehe 6
April 2023 mpaka tarehe 30 September 2023.

Warsha kabla ya uwasilishaji: UNCDF itaandaa warsha ya siku moja ili kutoa fursa kwa
waombaji (watakaopenda) kupata maelezo zaidi juu ya mwongozo wa maombi na kutoa fursa kwa
waombaji kuuliza maswali. Ikiwa unataka kushiriki warsha hii, tafadhali tuma barua pepe kwa
[email protected] yenye kichwa cha habari “Warsha ya CookFund”. Tafadhali onyesha
mkoa unakofanyia kazi zako (yaani, Dar es Salaam, Morogoro, Pwani, Dodoma na Mwanza).

Tarehe na ukumbi wa warsha vitathibitishwa kwa washiriki. Waombaji watatakiwa kubeba
gharama zao wenyewe za kuhudhuria warsha hii.

Angalizo: Kuhudhuria katika warsha hii sio sehemu ya masharti/vigezo vya kutuma maombi ya
ufadhili.

Kwa taarifa zaidi au maswali, tafadhali wasiliana na:

UNCDF Tanzania, Barua pepe: [email protected]
Tel: +255 22 260 0911

WhatsApp
Twitter
Email
LinkedIn
Instagram

Related