TANGAZO LA MNADA WA HADHARA WA VIFAA CHAKAVU
JUMATATU TAREHE 10.10.2022
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) inatarajia kuuza kwa mnada
wa hadhara vifaa chakavu vya aina mbalimbali jumatatu 10/10/2022.
Mnada utafanyika katika ofisi ya Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini
(GPSA) Mkoa wa Pwani iliyopo katika eneo la ujenzi karibu na kituo cha
mabasi cha Mkoa wa Pwani (Kibaha). Vitu vitakavyouzwa ni:
i. Vifaa vya TEHAMA (Photocopiers, printers, scanners, computers, Ups, n.k).
ii. Samani za aina mbalimbali (Viti, Meza n.k) na
iii. Vifaa vinginevyo (viyoyozi, n.k).
MASHARTI YA MNADA
i. Mnunuzi wa vifaa atatakiwa kulipia kifaa alichopata baada ya
kutangazwa na dalali kuwa ni mshindi.
ii. Kifaaambachohakitalipiwa kitanadiwa upya kabla mnada haujaisha.
iii. Mnunuzi atatakiwa kuchukua kifaa alichonunua mara tu baada ya kulipia (Cash).
iv. Watakaopenda kuona vifaa hivyo, wataruhusiwa siku mbili (2) kabla ya mnada.
Tafadhali kumbuka kuwa vifaa vitauzwa kama vilivyo na mahali vilipo. imetolewa na:
Mkurugenzi Mkuu,
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa