IMG-20231114-WA0006

GGML yapewa tuzo kampuni inayoaminika na walaji

WhatsApp
Twitter
Email
LinkedIn
Instagram

GEITA Gold Mining Limited (GGML) imeibuka kuwa kampuni inayoaminika zaidi kwenye sekta ya madini katika tuzo za mlaji (Consumer’s Choice Awards Africa) zilizotolewa mwisho mwa wiki iliyopita.

Akizungumza baada ya kupokea tuzo hizo zilizofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa GGML, Stephen Mhando alisema, “Tuzo hii ni uthibitisho wa kazi bora na muhimu tunayoifanya nchi nzima. Moja ya maadili yetu ya msingi ni kuhakikisha kuwa jamii inanufaika kutokana na uwepo wa GGML katika eneo hilo.

Dk. Biteko amewapongeza waandaaji wa Tuzo hizo ambazo sasa zinafanyika kwa mwaka wa Tano. Pia amepongeza washindi wote kwa kutoa huduma bora na kuzalisha bidhaa bora.
Naye Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Ashatu Kijaji alisema tuzo hizo  ni muhimu kwani zinakumbusha umuhimu wa wazalishaji, watoa huduma na wafanyabiashara kumjali yule anayepokea bidhaa yao au huduma yao.

Alisema tuzo hizo zimechangia katika uboreshaji wa utoaji wa huduma na bidhaa mbalimbali zinazoenda sokoni hivyo amewapongeza waandaaji wa Tuzo hizo ambazo sasa zimefikia mwaka wa Tano huku wigo wake ukiongezeka  kutoka  ndani ya Tanzania pekee na sasa ni Afrika kwa ujumla.

WhatsApp
Twitter
Email
LinkedIn
Instagram

Related