download

MJAMZITO AFARIKI KWA KUKOSA PESA, WATUMISHI WATATU WASIMAMISHWA TANGA.

WhatsApp
Twitter
Email
LinkedIn
Instagram

Mama mjamzito, Mariam Zahoro (30) Mkazi wa Kijiji cha Mumbwi Wilayani Handeni, Tanga amefariki dunia akiwa kwenye Kituo cha Afya Kabuku kilichopo Wilayani humo ikidaiwa kuwa alikosa huduma ya upasuaji baada ya kushindwa kulipa Tsh. 150,000 alizotakiwa kutoa kwa ajili ya huduma hiyo.

“Nilinyanyasika nikatukanwa kama mbwa alitakiwa kufanyiwa operesheni hawakuweza kumfanyia kwasababu hatukuwa na hela na Mimi ni fukara, Mwanangu aliniita akasema Mama njoo hapa nakufa sasa Mimi sina uwezo nikakaa pale akawa anasema Mama nishike mkono, Mama nishike kichwa, nililala chini sikuwa na cha kufanya akanipa mkono akaniambia Mama nakufa ndipo alipofariki”

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema amepokea kwa masikitiko habari za kifo cha mjamzito na kichanga chake, kilichotokea Handeni Tanga November 11,2023 katika Kituo cha Afya Kabuku kwa kinachoelezwa kuwa chanzo ni uzembe wa Watumishi wa Kituo hicho ambapo amesema tayari Watumishi watatu wamesimamishwa kazi kupisha uchunguzi.

Ummy amesema “Tayari Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Waziri Kindamba ametuma Timu kutoka Ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa inayojumuisha Madaktari bingwa wawili (Daktari Bingwa wa Wanawake na Uzazi na Daktari Bingwa wa Huduma za Usingizi ) ili kufanya uchunguzi wa tukio hili”

WhatsApp
Twitter
Email
LinkedIn
Instagram

Related