Crude Oil Pipeline-EACOP

MAOMBI YA KUWASILISHA NIA KWA AJILI YA UTOAJI HUDUMA ZA UTHAMINI KATIKA MRADI WA BOMBA LA MAFUTA GHAFI LA AFRIKA MASHARIKI (EACOP) KUMB NA – REQ-00000094

WhatsApp
Twitter
Email
LinkedIn
Instagram

Kampuni ya EACOP inazialika kampuni zenye uzoefu na sifa kuwasilisha maombi ya nia ya kutoa
huduma za uthamini katika Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP).

Mradi wa EACOP unahusisha ujenzi na uendeshaji wa bomba litalofukiwa ardhini, linalokatisha
mipaka ya nchi mbili ili kusafirisha mafuta ghafi kutoka eneo la Ziwa Albert nchini Uganda hadi
Pwani ya Mashariki mwa Tanzania kwa ajili ya Kwenda katika Masoko ya Kimataifa. Bomba
litaanzia eneo la Kabaale Wilaya ya Hoima, nchini Uganda, hadi eneo la Chongoleani, Mkoani
Tanga nchini Tanzania.

MAELEZO MAFUPI YA MAWANDA YA HUDUMA:
Utwaaji wa kudumu wa ardhi inayohitajika na Mradi wa EACOP unaelekea kukamilika. Wakati
wa kipindi cha ujenzi, Wakandarasi wa Ujenzi watahitaji ardhi ya ziada ili kuitumia kwa muda
kufanya kazi mbalimbali kando kando mwa mkuza wote wa Bomba la Mafuta. Hivyo, kampuni ya
EACOP itahitaji kufanya makubaliano ya kutumika ardhi kwa muda ikihusisha vipande vya ardhi
zaidi ya 250, vinavyokadiriwa kuwa na ukubwa wa kati ya ekari 0.5 hadi 1.25. Kampuni ya
EACOP inatafuta kampuni yenye uzoefu wa kutosha ili kuwezesha mchakato wa kupatikana ardhi
ya muda itakayotumika kufanyia kazi kwa muda kando kando ya mkuza wa Bomba la Mafuta au
kwa shughuli nyingine zozote za maandalizi ya Ujenzi.

Mawanda ya huduma yatahusisha;
 Kuthibitisha mahitaji ya ardhi ya muda na Timu za Ardhi na Uhandisi za EACOP katika
kila eneo husika
 Kuzingatia matakwa ya ardhi ya muda kama yanavyoelezwa kwa kina katika Mpango wa
Usimamizi wa Ardhi wa EACOP
 Kubainisha ardhi na wamiliki wake na kuwashirikisha kuhusu uhitaji wa kutumia ardhi hizo
kwa muda
 Kufanya tathmini ya hali ya ardhi kabla na baada ya kutumia ardhi hiyo kwa muda.
 Kufanya makubaliano na wamiliki wa ardhi na watumiaji ili kutumika ardhi hizo kwa muda

VIGEZO MUHIMU:
Kampuni zinazowasilisha nia zinapaswa kutuma maombi pamoja na nyaraka zifuatazo::

Uthibitisho wa Usajili kama Kampuni ya Uthamini toka Bodi wa ya Usajili Wathamini.
 Uthibitisho wa Usajili wa Wathamini wa Kampuni hiyo ya toka Bodi ya Usajili wa
Wathamini.
 Maelezo mafupi kuhusu uzoefu wa kutoa huduma za uthamini chini ya sheria za Tanzania
na Viwango vya Fedha Kimataifa kwenye miradi mikubwa nchini Tanzania na maeneo ya
vijijini
 Leseni ya biashara.
 Uthibitisho wa Usajili toka Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA) na Cheti cha
Uthibitisho wa Malipo ya Kodi cha mwaka wa hivi karibuni.
 Usajili katika Kanzi Data ya Watoa Huduma wa Ndani ya EWURA (LSSP) au ushahidi
thabiti wa maombi ya usajili wakati wa uwasilishaji wa maombi ya nia hii iliyotangazwa.
 Kufuata/kukubaliana na kanuni za Wazawa za Mambo ya Petroli za Tanzania.
 Wasifu wa watendaji watakaohusika katika Mradi ikiwa ni pamoja na nakala za vyeti vyao,
kiwango cha elimu, uzoefu na uwezo wa kutoa huduma inayohitajika.
 Uwezo wa kifedha wa kutoa huduma zinazohitajika ikiwa ni Pamoja na kuwakilisha hesabu
za fedha za miaka mitatu iliyopita.
 Uthibitisho kutoka mfumo wa usimamizi wa QHSE, taasisi na mchakato kulingana na
viwango vya ndani na vya ki-sekta vinayotumika kwa kazi hii.
 Uthibitisho wa kukubaliana na sera za kupinga rushwa, ufisadi ma Haki za Binadamu.

Kampuni zenye nia uwezo na rasilimali ya kutoa huduma zilizotajwa hapo juu zinatakiwa kutuma
maombi ya nia yaliyoandaliwa kwa lugha ya Kiingereza pamoja na nyaraka zilizobainishwa hapo
juu kupitiabarua pepe: [email protected] (ukubwa usiozidi MB20) kabla au si zaidi ya
saa 11:00 jioni Majira ya Afrika Mashariki, tarehe Jumatano 15 Februari 2023. Kichwa cha cha
barua pepe kiwe: [REQ-00000094] Kutoa huduma za uthamini katika Mradi wa EACOP.

Maombi yote ya kuonesha nia yawe kati ya kurasa 10 hadi 20.

Maombi yote lazima yawasilishwe kwa lugha ya Kiingereza.

Muhimu: EACOP itapitia na kuchambua nyaraka ziizotumwa na makampuni yalioonesha nia
kulingana na EOI hii, na kisha kufanya tathmini kulighana na vigezo vya ndani vya EACOP ili
kubaini makampuni yenye sifa yatakayojumuishwa kwenye orodha ya awali ya makampuni yenye
vigezo. Mwaliko kwa Makampuni kutuma maombi ya zabuni utatumwa kwa Makampuni ya awali
yenye vigezo baada ya makampuni hayo kusaini Makubaliano ya Utunzaji wa Taarifa (NDA).
Kampuni ya EACOP LTD ina haki ya kuteua au kukataa kampuni na kubaki na maamuzi yake bila
kutoa sababu kwa kampuni husika

WhatsApp
Twitter
Email
LinkedIn
Instagram

Related