OMBI LA KUONESHA NIA YA KUTOA HUDUMA ZA USAFIRI WA NDEGE KWA WAFANYAKAZI
KUMBUKUMBU NA: 10007995
Kampuni ya Mafuta Gha ya Afrika Mashariki (EACOP) Ltd, ambayo ni Kampuni ya mafuta na gesi, inaalika kampuni au taasisi zenye uzoefu na weledi wa kutosha kuonesha nia ya kutoa huduma ya usari wa ndege kwenda kwenye Mradi wa bomba la mafuta gha la Afrika mashariki.
Mradi wa EACOP unajumuisha ujenzi na uendeshaji wa bomba la kusarisha Mafuta lililofukiwa chini ya ardhi linalokatisha mipaka ya nchi mbili na litakalo sarisha mafuta kutoka eneo la Ziwa Albert nchini Uganda mpaka mashariki mwa pwani ya Tanzania kwa ajili ya kusarisha Mafuta katika masoko ya kimataifa. Bomba litaanzia Kabaale katika Wilaya ya Hoima, nchini Uganda, mpaka Chongoleani, Mkoa waTanga nchini Tanzania. Urefu wa bomba ni kilomita 1,443, kati yake kilomita 1,147 zitakuwa nchini Tanzania.
MAELEZO MAFUPI YA HUDUMA:
Huduma za Usari wa Ndege:
• Sifa Husika za ndege: Ijulikanayo kitaalamu kama xed wing, Marubani 2, Injini pacha, Iwe na injini yenye
turubo ya kusukuma propela , iwe inazingatia vigezo vya Mamlaka ya Kimataifa ya Usarishaji wa Anga.
• Viwanja vya Ndege: Dar-es salaam/Tanga au mahali pengine penye kiwanja cha ndege (Kiwanja chenye
moramu).
• Ratiba: Safari 2 za Kwenda na kurudi kwa wiki kwenye viwanja vya ndege vilivyotajwa. Safari za kawaida
za ndege za abiria zinaweza kuruhusiwa baadae.
• Ratiba ya kuanza: Inakadiriwa kuanza tarehe 1 Desemba 2022.
• Mshahara: Unajumuisha viwango vyote vya malipo kwa kila saa ya kuruka angani.
• Muda: Mwaka mmoja ingawa unaweza kuongezeka
VIGEZO MUHIMU:
Makampuni au taasisi zinzoonesha nia zanaalikwa kutuma maombi na kuambatanisha nyaraka zifuatazo:
• Uthibitisho wa usajili wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na cheti cha uthibitisho wa mlipa kodi kwa
mwaka wa fedha uliopita.
• Inashauriwa kuwasilisha maombi ya usajili kwenye kanzi data ya EWURA ya Watoa Huduma ya Ugavi wa
Ndani (LSSP) wakati wa konesha nia.
• Kuzingatia kanuni za watoa huduma wa ndani za mwaka 2017 na ufafanuzi wa makampuni ya ndani.
• Uzoefu, utendaji na uwezo wa kutoa huduma zilizoorodheshwa hapo juu katika kiwango kikubwa nchini
Tanzania, kulingana na viwango vya kitaifa na kimataifa.
• Uwezo wa kifedha wa kutoa huduma zinazohitajika ikiwa ni pamoja na kuwasilisha hesabu za fedha za
mwaka husika.
• Uthibitisho kutoka kwenye mfumo wa Usimamizi wa QHSE, taasisi na mchakato kulingana na Viwango vya
Ndani na vya Ki-Sekta vinavyotumika kwa kazi hii.
• Leseni ya biashara kutoka nchii husika inayothibitisha kufanya kazi hii.
• Vyeti vya ubora wa ndege.
• Wasifu wa marubani na marubani wasaidizi pamoja na wahudumu wengine watakaohusika katika kutoa
huduma, ikiwa ni pamoja na vyeti vya lazima vya kila mhudumu, viwango vya elimu, ushahidi wa mafuzo ya
mara kwa mara.
• Uthibitisho mwingine wowote wa Kampuni, vibali na leseni.
• Uthibitisho wa kukubaliana na sera za kupinga rushwa, usadi, na Haki za Binandamu.
Kampuni zenye nia, ambazo zina uwezo na rasilimali za kutosha kutoa huduma zilizotajwa hapo juu zinapaswa
k u t u m a m a o m b i n a k u a m b a t a n i s h a n y a r a k a z i l i z o t a j w a h a p o j u u k u p i t i a b a r u a p e p e y a [email protected] (ukubwa wa barua pepe usizidi 20Mb) mnamo au kabla ya Tarehe
1 Novemba 2022 saa 12:00 jioni saa za Afrika Mashariki (EAT). Kichwa cha Barua pepe kiwe
1007995.
Maombi yote yakuonesha nia yasizidi kurasa 10 hadi 20.
Maombi yote lazima yawasilishwe kwa lugha ya Kingereza.
Muhimu: Mradi wa EACOP utapitia na kuchambua nyaraka zilizotumwa na makampuni yenye nia Kwa ajili ya kutengeneza orodha ya (Makampuni) ya awali yenye vigezo. Mwaliko wa Makampuni kutuma maombi ya zabuni utatumwa kwa makampuni ya awali yenye vigezo baada ya makampuni hayo kusaini Makubaliano ya Utunzaji waTaarifa (NDA).