LOGO

Tangazo la Uwekezaji Katika Eneo la Stendi Hospitali ya Taifa ya Muhimbili – Mlonganzila katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo

WhatsApp
Twitter
Email
LinkedIn
Instagram

HALMASHAURI YA MANISPAA YA UBUNGO

TANGAZO LA MWALIKO

Tarehe 25 Juni , 2019

1. Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo imejenga stendi katika eneo la Mlonganzila karibu na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, kuokana na hilo, kuna huduma za jamii zinazohitajika kwa ajili ya kuhudumia watumiaji wa stendi hiyo.

2. Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo inawakaribisha wawekezaji mbalimbali kujitokeza ili kujenga maduka kwenye stendi hiyo. Zifuatazo ni biashara ambazo wawekezaji wanaweza kuwekeza kwenye stendi hiyo:

Lot Na BIASHARA IDADI
1 Maduka ya dawa 3
2 Maduka ya vinywaji jumla 15
3 Kontena za futi 40 5
4 Kontena za futi 20 8
5 Fremu za mama lishe 8
6 Fremu za wafanya biashara wa matunda 5
7 Fremu za shajala (stationary) 3
8 Maduka ya vinywaji vya rejareja 5
9 Vibanda vya huduma ya fedha 5
10 Duka la nyama/samaki nk 1
11 Min Supermarket 2
12 Restaurant 2
13 Ofisi 3

3. VIGEZO VYA WAOMBAJI:
3.1 Awe na kitambulisho cha uraia
3.2 Awe na leseni ya biashara husika
3.3 Awe na uwezo wa kujenga duka hilo kulingana na mchoro, alama tambuzi na mchanganuo wa gharama watakazopewa au kuweka kontena kulingana na ukubwa ulioainishwa.
3.4 Awe tayari kuingia mkataba na Halmashauri wa jenga, endesha, kabidhi kulingana na vigezo vitakavyo wekwa.

4. Wawekezaji wanaweza kukagua nyaraka kupata maelezo kutoka kwa Mhandisi wa Ujenzi Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo S.L.P. 55068 Dar es Salaam, Ubungo siku ya Jumatatu hadi Ijumaa isipokuwa siku za Sikukuu za Kitaifa kuanzia saa tatu hadi saa tisa na nusu jioni.

5. Nyaraka zinapatikana kwa kuleta barua ya maombi na malipo ya fedha taslimu yasiyorudishwa (Non – refundable) ya 50,000/= gharama hizo ni kwa kila “Lot” kwa Mkurugenzi wa Manispaa S.L.P. 55068 Ubungo.

6. Nyaraka zote ziwe na nakala halisi (original) moja (1) na nakala kivuli moja (1) zinazofanana, zilizojazwa kwa usahihi na zilizowekwa kwenye bahasha isiyo na maandishi juu na kuandikwa LOT No. …………. uwekezaji wa……………………………………………………….. Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo. Ni lazima kupelekwa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo kwa anuani ifuatayo:-

Mkurugenzi wa Halmashauri,
Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo,
S.L.P 55068
UBUNGO.

7. Siku ya mwisho ya kuwasilisha nyaraka ni tarehe 09 Julai, 2019 saa sita kamili mchana zitafunguliwa kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo tarehe 09 Julai 2019 saa sita na nusu mchana, mbele ya wawekezaji au wawakilishi wao wanaoamua kuhudhuria katika ufunguaji wa zabuni.

8. Nyaraka zitakazochelewa, sehemu ya Nyaraka, Nyaraka za kielektroniki, na Nyaraka zisizofunguliwa katika tukio la ufunguaji Nyaraka, kwa hali yoyote ile Nyaraka hizo hazitakubaliwa..

MKURUGENZI WA MANISPAA
HALMASHAURI YA MANISPAA YA UBUNGO.

WhatsApp
Twitter
Email
LinkedIn
Instagram

Related