LOGO

Tangazo la Zabuni Halmashauri ya Mji wa Mafinga

WhatsApp
Twitter
Email
LinkedIn
Instagram

HALMASHAURI YA MJI WA MAFINGA

(Barua zote ziandikwe kupitia kwa Mkurugenzi wa Mji)
MKOA WA IRINGA

Tangazo kwa ajili ya kupata wazabuni tarajali kwa ajili ya kutoa huduma mbalimbali NDANI YA HALMASHAURI YA MJI KWA KIPINDI CHA MWAKA WA FEDHA 2019/2020
1) Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mafinga anawatangazia Wafanyabiashara, Wananchi, Wakandarasi wote wenye sifa na uwezo wa kutoa huduma mbalimbali kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2019/2020 watume maombi yao kulingana na mahitaji yaliyoainishwa hapa chini:-

A. BIDHAA NA HUDUMA MBALIMBALI
S/NO NAMBA YA HUDUMA MAELEZO YA HUDUMA INAYOHITAJIKA

  1. LGA.169/2018/2019/G/1 HUDUMA YA UUZAJI WA MAFUTA, DIESEL, PETROL, MAFUTA YA TAA, VILAINISHI.
  2. LGA.169/2018/2019/G/2 HUDUMA YA VIFAA VYA KILIMO NA PEMBEJEO

B. ZABUNI ZA WAKALA WA UKUSANYAJI WA USHURU

  1. LGA.169/2018/2019/NCS/1 UKUSANYAJI WA USHURU WA CHOO CHA SOKONI

C. ZABUNI YA UTENGENEZAJI WA VIFAA TIBA

  1. LGA.169/2018/2019/NCS/2 UTENGENEZAJI WA VIFAA TIBA

D. UKODISHAJI WA VYUMBA VYA BIASHARA

  1. LGA.169/2018/2019/NCS/3 CHUMBA NA.64 SOKO KUU –MAFINGA
  2. LGA.169/2018/2019/NCS/4 CHUMBA NA.65 SOKO KUU – MAFINGA
  3. LGA.169/2018/2019/NCS/5 JENGO LA MGAHAWA (CHUMBA NA.290) SOKO KUU – MAFINGA
  4. LGA.169/2018/2019/NCS/6 VYUMBA HAMSINI (50) VYA BIASHARA VILIVYOPO ENEO LA SOKO KUU MAFINGA

(2) Dhana ya pre-qualification Notice kama ilivyoainishwa kwenye sheria ya manunuzi ni kupata watoa huduma Wakandarasi. Wafanya Biashara (Suppliers) wenye uwezo watakao kamilisha masharti yaliyoainishwa kuweza kutoa huduma ndani ya Halmashauri ya Mji wa Mafinga mwaka wa fedha 2019/2020.

(3) Tangazo hili la kupata Wazabuni tarajali liko wazi kwa Suppliers/Contractors and Service Providers kuomba kulingana na aina biashara anayoiona anaiweza.

(4) Pre-qualification itafanyika kwa ajili ya ushindani wa ki-taifa (National Competitive bidding procedure specified in the Public Procurement (Goods, works, Non-Consultant Services and Disposal of Public Assets by tender) Regulation 2013 na marekebisho yake ya Mwaka 2016

(5) Wazabuni ni lazima ainishe bayana ilipo Ofisi yake Plot no. na Jina la Mtaa.

(6) Kwa watakaoomba ukusanyaji ushuru ni lazima ataje kiwango atakachokusanya kwa mwezi na Asilimia ya marejesho yake atakayolipwa na Halmashauri kama Fomu ya maoteo inavyoelekeza kama akiteuliwa.(Maelezo zaidi yanapatikana kwenye kitabu cha zabuni)

( 7) Kwa waombaji wa kundi ‘’C’’ anatakiwa azingatie mambo yafuatayo,

  • Muombaji ataje namba ya chumba anachoomba.
  • Muombaji asiwe anadaiwa na Halmashauri ya Mji wa Mafinga.

(8) Tathimini itazingatia Masharti yaliyoainishwa kwenye Tangazo na Kitabu cha Zabuni husika.

(9) Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 25.05.2019 saa 6 kamili Mchana. Maombi yote yakiwa yamefungwa kwenye bahasha yenye lakiri na isiyo na alama ya kumtambulisha aliyeomba. Yanatakiwa yawe yameshatumwa kwa Register au kuletwa kwa mkono kwenye Ofisi ya Mkurugenzi wa Mji wa Mafinga iliyopo Jengo la HIMA, S.L.P. 76 Mafinga kabla na si zaidi ya saa 6.00 Mchana tarehe 25.05.2019 na ufunguzi utafanyika mara tu mwisho wa saa na tarehe tajwa hapo juu kukamilika.

(10) Kila atakayeomba ni lazima aonyeshe aina ya Huduma aliyoomba juu ya bahasha na aonyeshe kwa maandishi isifunguliwe hadi tarehe 25.5.2019 ieleweke kuwa asipoainisha aina ya Huduma aliyoombea Zabuni hiyo haitafikiriwa na wala haitafunguliwa.

(11) Zabuni zitakazoletwa baada ya muda kuisha hazitapokelewa na wala kufunguliwa.

(12) Watumishi wa Halmashauri pamoja na Waheshimia Madiwani hawaruhusiwi kuomba Zabuni hizi.

(13) Ada ya mchakato huu wa Wazabuni tarajali ni shilingi za Kitanzania Laki moja tu (100,000/= ) kwa Jedwali A na B na C na kiasi cha shilingi Elfu hamsini (50,000/=) kwa ukodishaji wa vyumba vya biashara ambazo hazirejeshwi. Na zinapaswa kulipwa kwenye Ofisi ya Mhasibu Mkuu Halmashauri ya Mji wa Mafinga kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa tisa kamili jioni siku za kazi, kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa kila huduma utakayoomba inajitegemea.

VOSTER MGINA
KAIMU MKURUGENZI
HALMASHAURI YA MJI WA MAFINGA

Simu Na.026-2772393
Fax No. 026- 2772070
Mkurugenzi wa Mji
S.L.P 76 MAFINGA
11.05.2019

Valid from : 14/05/19 – 25/05/19

Source: Mwananchi

WhatsApp
Twitter
Email
LinkedIn
Instagram

Related