KTO

Tangazo la Zabuni Karibu Tanzania Organization

WhatsApp
Twitter
Email
LinkedIn
Instagram

KARIBU TANZANIA ORGANIZATION

TANGAZO LA ZABUNI

Karibu Tanzania Organization, inatangaza Zabuni zifuatazo;

1.Huduma ya chakula.

Muombaji anatakiwa kutimiza vigezo vifuatavyo;

·         Kuwa tayari kutoa huduma ya chakula (catering services) kwenye eneo atakalopangiwa kwa Kuzingatia kanuni za Afya na usalama wa walaji.

·         Awe na uzoefu wa kutoa huduma hiyo usiopungua miaka 2 katika taasisi zinazotambulika na asiwe na mgongano wa kimaslahi na shirika.

·         iAwe na leseni halali ya biashara inayohusiana na shughuli hizo na Cheti cha uthibitisho wa kutoa huduma hiyo kutoka kwa mamlaka ya chakula na dawa (TMDA).

·         Awe tayari kuthibitisha uwezo wa kitaaluma wa kutoa huduma ya chakula.

·         Awe tayari kuthibitisha uwezo wa kifedha aiionao wa kuendesha shughuli hizo kwa ufanisi.

2. Madereva wa muda mfupi (Parttime) Nafasi tatu Muombaji anatakiwa kutimiza vigezo vifuatavyo;

·         Awe na Leseni halali pamoja na Cheti kutoka chuo Kinachotambuiika .

·         Awe na uzoefu usiopungua miaka 2.

·         Awe na-afya njema, akili timamu, mwadilifu, mbunifu na anayeweza kujisimamia mwenyewe katika kutimiza majukumu atakayopangiwa.

3. Afisa Tehama na Ubunifu IT & Graphics designer (Parttime) Muombaji anatakiwa kutimiza vigezo vifuatavyo;

·         Awe na uwezo wa kusimamia shughuli zote za Tehama ikiwemo matengenezo

·         Awe na uwezo wa kutengeneza na kusasisha (Update) tovuti.

·         Awe mbunifu na mwenye uwezo wa kuunda dhana mpya za ubunifupicha na mpangilio (new design concepts, graphics and layout).

·         Awe na Cheti kutoka Chuo kinachotambulika na uzoefu usiopungua mwaka 1

4. Msanifu wa Ndani wa Ofisi na Matengenezo -lnterior Designer Muombaji anatakiwa awe na Sifa zifuatazo:

·         Awe na uwezo wa kutumia ubunifu na utaalamu katika kupangilia ofisi na Samani zake.

·         Awe na utaalamu na Uzoefu katika Matengenezo na marekebisho ya Ofisi.

·         Awe na Leseni ya biashara, Uzoefu usio pungua miaka 2. na Ushahidi wa kufanya kazi za Usanifu wa Ndani pamoja na Matengenezo.

Maombi yawasilishwe kwa Mkurugenzi, KARIBU TANZANIA ORGANIZATION, S.L.P. 246, Muccadam Building, Upanga Dar es salaam au kwa barua pepe: [email protected]  Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 6/11/2019

Chanzo; Mwananchi

WhatsApp
Twitter
Email
LinkedIn
Instagram

Related