LOGO

Tangazo La Zabuni Wakala Wa Kukusanya Kodi Katika Nyumba Za Kulala Wageni

WhatsApp
Twitter
Email
LinkedIn
Instagram

HALMASHAURI YA MANISAPAA YA ILALA

TANGAZO LA ZABUNI

WAKALA WA KUKUSANYA KODI KATIKA NYUMBA ZA KULALA WAGENI

ZABUNI NAMBA: LGA/O15/2019-2020/HQ/NCS/35

1.Halmashauri ya Manispaa ya llala inakusudia kuweka Wakala wa kukusanya kodi katika nyumba za kulala wageni (Hotel Levy) kwa kipindi cha Mwaka mmoja.

2.Halmashauri ya Manispaa ya llala inapenda kuwaalika watu Binafsi, Makampuni, Mashirika, Taasisi au vikundi vya watu vilivyosajiliwa kisheria, wenye nia na uwezo wa kufanya kazi hiyo Ya uwakala katika kata 36 za Manispaa ya llala.

3. Zabuni hizi zipo wazi kwa wananchi na wakazi wote wa Tahzania na zitaendeshwa kwa mujibu wa sheria na kanuni za manunuzi ya Umma (Bidhaa, ujenzi, huduma zisizo za kiushauri na uteketezaji wa mali chakavu za Umma kwa zabuni) sheria namba 07 (2011) na kanuni zake za mwaka, 2013 G.No 446

4. Wazabuni wote wanaokusudia kuomba zabuni hizi na walio na sifa zinazotakiwa wanaweza kuflka na kupata taarifa zaidi pamoja na kukagua nyaraka za zabuni husika oflsini kwa katibu wa Bodi ya Zabuni ya Halmashauri kwa gharama zao wenyewe kuanzia Jumafatu saa 2:00 asubuhi hadi Ijumaa saa 9:30jioni 1 isipokuwa siku za siku kuu tu.

5. Fomu maalumu za maombi au nyaraka za zabuni zimeandaliwa kwa lugha ya Kiswahili na zinauzwa Tsh 50,000/=,Kabla ya kuchukua fomu utapaswa kuleta barua kwa anwani tajwa hapojuu ukieleza unahitaji zabuni gani. Pesa ya maombi ya zabuni hazitarudishwa.

6. Maombi yote yajazwe kwa makini na yaambatane na nakala mbili (original + copies) na yafungwe vizuri kwa rakili ndani ya bahasha, yatumwe kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala S.L.P 20950 Dar es  salaam kabla ya tarehe 22 Oktoba 2019 saa 4.00 asubuhi. Zabuni zitafunguliwa siku hiyo hiyo saa 4.30 Asubuhi mbele ya waombaji wote/wawakilishi wao watakaopenda kuhudhuria katika tafrija ya ufunguzi itakayofanyika katika Ofisi za manunuzi zilizopo Kamata Depot Sambamba na ”MKUKI HOUSE” Juu ya bahasha iandikwe aina ya zabuni na namba yake iliyoombewa na SIYO JINA LA MWOMBAJI: Mfano: Uwakala wa kukusanya Kodi ya Nyumba za kulala Wageni (Hotel Levy) , Zabuni Na. LGA/015/IMC/2019-2020/NCS/35 LOT …………

7. Zabuni zitakazochelewa kufika kwa muda uliopangwa, sehemu ya Zabuni zitakazotumwa kwa njia ya elektroniki, mfano faksi, barua pepe nk, zabuni ambazo hazikufunguliwa siku ya ufunguzi na zabuni ambazo hazikupokelewa hazitakubaliwa kufanyiwa tathmini bila kujali mazingira yeyote.

8. Tathmini itazingatia vigezo vyote vilivyopo kwenye nyaraka ya zabuni, pamoja na bei kulingana na bajeti Ya Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2019/2020.

9. Wakala atakusanya Ada katika Nyumba za kulala wageni kila siku na atawasilisha Halmashauri mapato  Ya kila siku,katika Akaunti Namba 0150251270100 CRDB au 20160019984 NMB Morogoro Road Branch. Jina la Akaunti ni Mkurugenzi wa Manispaa ya llala na atalipwa kamisheni kutoka katika makusanyo aliyowasilisha baada ya kuwasilisha hati ya madai kwa Mkurugenzi.

JUMANNE K. SHAURI
MKURUGENZI WA MANISPAA
HALMASHAURI YA MANISPAA YA ILALA

WhatsApp
Twitter
Email
LinkedIn
Instagram

Related