LOGO

Tangazo la Zabuni ya Wakala wa Utozaji wa Ada za Maegesho ya Vyombo vya Usafiri kwenye Hifadhi za Barabara Halmashauri ya Wilaya ya Igunga, Halmashauri ya Wilaya ya Mji wa Nzega, Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Halmashauri ya Manispaa ya Tabora na Halmashauri ya Wilaya ya Urambo Mkoa wa Tabora

WhatsApp
Twitter
Email
LinkedIn
Instagram

TANGAZO LA ZABUNI

ZABUNI NA. AE/092/2019/2020/TBR/NC/01-05

YA

WAKALA WA UTOZAJI WA ADA ZA MAEGESHO YA VYOMBO VYA USAFIRI KWENYE HIFADHI ZA BARABARA HALMASHAURI YA WILAYA YA IGUNGA, HALMASHAURI YA MJI WA NZEGA, HALMASHAURI YA WILAYA YA SIKONGE, HALMASHAURI YA MANISPAA YA TABORA NA HALMASHAURI YA WILAYA YA URAMBO MKOA WA TABORA

Tarehe: 23/05/ 2019

1. Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini Tanzania (TARURA) Mkoa wa Tabora unakusudia kutumia huduma za Wakala kutoza ada za maegesho ya vyombo vya usafiri katika maeneo ya hifadhi za barabara zote zilizo chini ya usimamizi wake katika Halmashauri ya Wilaya ya Igunga, Halmashauri ya Mji wa Nzega, Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Halmashauri ya Manispaa ya Tabora na Halmashauri ya Wilaya ya Urambo

2. Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini Tanzania (TARURA) Inapenda kuwakaribisha waombaji wenye sifa kutuma maombi kwa ajili ya zabuni ya wakala wa kutoza Ada za maegesho ya vyombo vya usafiri kwenye hifadhi za barabara katika halmashauri ya Wilaya ya Igunga, Halmashauri ya Mji wa Nzega, Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Halmashauri ya Manispaa ya Tabora na Halmashauri ya Wilaya ya Urambo, Zabuni Namba. AE/092/2019/2020/TBR/NC/01-05

3. SIFA ZA MUOMBAJI: Muombaji atatakiwa kuwa na sifa zifuatazo

i. Awe Mtanzania
ii. Muombaji awe ni Kampuni iliyosajiliwa kwa mujibu wa Sheria za Tanzania na ambayo haijawahi kuzuiwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) kujihusisha na shughuli za Ununuzi wa Umma.
iii. Muombaji awe na mtaji usiopungua Shilingi Milioni Mia Moja (100, 000,000.00) ambao umeainishwa kwenye Memorandamu ya Kampuni (Memorandum and Articles of Association) au ushahidi kuwa kampuni iliongeza mtaji wake.
iv. Muombaji awe na ofisi ya kudumu anapofanyia kazi zake.
v. Muombaji awe na leseni hai ya biashara ya uwakala wa utozaji wa ada ya maegesho.
vi. Muombaji awe na uzoefu usiopungua miaka miwili kwenye kazi ya uwakala wa utozaji wa ada ya maegesho ya Vyombo vya Usafiri kwaniaba ya Mamlaka za Serikali za Mitaa hususani Majiji, Manispaa au Taasisi za Serikali.
vii. Muombaji awe na cheti cha Utambulisho wa Mlipakodi (TIN)
viii. Muombaji awe amesajiliwa kulipa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT)
ix. Muombaji awe na hati halali ya kuthibitisha ulipaji wa kodi (Tax Clearance)
x. Muombaji awe na taarifa za kifedha zilizokaguliwa (Audited Financial Statement) kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia 2016 hadi 2018.
xi. Muombaji awe na taarifa za kifedha ya benki (Bank Statement) ya kipindi cha kuanzia tarehe 1 Januari, 2018 mpaka tarehe 30 Aprili, 2019 yenye mauzo (turnover) yasiyopungua kiasi kama ilivyoainishwa katika jedwali kwa kila Halmshauri atakayoomba:-

NA. WILAYA SHILINGI
1 MANISPAA YA TABORA 50,000,000.00
2 IGUNGA 10,000,000.00
3 MJI WA NZEGA 10,000.000.00
4 SIKONGE 10,000,000.00
5 URAMBO 10,000,000.00

Taarifa hiyo iwe na “Certificate of Balance” kutoka katika Benki husika.

xii. Muombaji awe na cheti cha OSHA kinachoonyesha kukidhi matakwa ya Sheria Na. 5 ya Mwaka 2003
xiii. Muombaji awe amesajiliwa kwenye Mfuko wa Fidia kwa wafanyakazi (WCF) kwa mujibu wa Sheria ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi Sura ya 263 pitio la Mwaka 2015.
xiv. Muombaji awe na sifa njema ya kufanya kazi ya Uwakala wa kukusanya ada za maegesho ya vyombo vya usafiri kwaniaba ya Mamlaka za Serikali za Mitaa hususani Majiji, Manispaa au Taasisi za Serikali
xv. Asiyewahi kuwa na mashauri katika chombo chochote cha Kisheria kuhusiana na mkataba wa aina yoyote na Taasisi yoyote ya Serikali.

4. Zabuni zitashughulikiwa kwa utaratibu wa ushindani wa kitaifa [National Competitive Bidding] ulioainishwa kwenye Kanuni za Ununuzi wa Umma za Mwaka 2013, zikisomwa pamoja na marekebisho yake ya Mwaka 2016 na zikiwa wazi kwa waombaji wote wa hapa nchini.

5. Waombaji wote wenye nia na uwezo wanaweza kupata taarifa kamili kupitia makabrasha ya zabuni katika ofisi ya Katibu wa Bodi Kasimu ya Zabuni TARURA Mkoa wa Tabora, kupitia anuani iliyotajwa kwenye jedwali hapo juu kila siku kuanzia saa mbili kamili (02.00) asubuhi hadi saa tisa (09:00) kamili alasiri, siku za Jumatatu hadi Ijumaa [isipokuwa siku za sikukuu zinazotambulika kitaifa].

6. Muombaji atatakiwa kujaza Kwa usahihi na kuwasilisha Fomu ya dhamana ya zabuni (Bid Securing Declaration) kwa muundo unaopatikana kwenye kabrasha la zabuni.

7. Nyaraka za Zabuni zitapatikana baada ya kulipa ada stahiki ya zabuni ya Shillingi Laki Moja tu (TZS 100,000.00) Kupitia akaunti namba 53010001080 iliyopo katika Benki ya NMB, TARURA Collection Account Muombaji atatakiwa kuwasilisha nakala halisi ya hati ya malipo ya Benki ikiambatana na barua ya maombi ya Zabuni husika. Malipo yaliyolipwa kama ada ya maombi ya zabuni hayatarejeshwa.

8. Zabuni zote ziwe na nakala halisi (original) moja (1) na nakala (copies) tatu (3) zinazofanana zifungwe ndani ya bahasha iliyofungwa kwa lakiri na juu ya bahasha ziandikwe maelezo ya Zabuni na kasha iandikwe na kuwasilishwa kwa anuani ifuatayo: Katibu wa Bodi Kasimu ya Zabuni TARURA Mkoa wa Tabora S. L. P.685, Kipalapala Kupitia Barabara Tabora Manispaa Kuelekea Sikonge (km 8) kutoka Standi kuu ya Mabasi).

9. Siku ya mwisho ya kuwasilisha maombi ya zabuni ni tarehe 06/06/2019 kabla ya saa 05:00 asubuhi. Zabuni zitafunguliwa hadharani mara tu baada ya muda wa mwisho wa kuwasilisha zabuni, waombaji wote au wawakilishi wao wanaalikwa kuhudhuria ufunguzi wa zabuni hizo utakaofanyika siku hiyo katika ofisi ya Mratibu wa TARURA Mkoa wa Tabora S. L. P.685, Kipalapala Kupitia Barabara Tabora Manispaa Kuelekea Sikonge (km 8) kutoka Standi kuu ya Mabasi).

10. Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini Tanzania (TARURA) hautalazimika kukubali/ kutokukubali kutoa zabuni kwa mwombaji yeyote kutokana na kigezo cha malipo makubwa/malipo kidogo ya zabuni.

11. Zabuni zitakazochelewa kuwasilishwa, zabuni za kielektroniki, na zabuni zisizofunguliwa katika tukio la ufunguaji zabuni, kwa hali yoyote ile hazita kubaliwa kwa tathmini.

Mhandisi Regnard Silanga
MRATIBU WA MKOA-TABORA
WAKALA WA BARABARA ZA VIJIJINI NA MIJINI TANZANIA (TARURA)

WhatsApp
Twitter
Email
LinkedIn
Instagram

Related