UBUNGO MANISPAA

Zabuni ya Uwakala wa Ukusanyaji wa Mapato Yatokanayo na Ada za Vyoo vya Umma Katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo

WhatsApp
Twitter
Email
LinkedIn
Instagram

HALMASHAURIYA MANISPAA YA UBUNGO

ZABUNI

NAMBA: LGA/180/2018 – 2019/ NCS/53

UWAKALA WA UKUSANYAJI WA MAPATO YATOKANAYO NA ADA ZA VYOO VYA UMMA KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA UBUNGO

Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo inakusudia kuweka mawakala kwa ajili ya ukusanyajl wa mapato yatokanayo na ada za vyoo vya Umma katlka masoko ya Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.

Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo inawakaribisha kuleta Zabuni zenu kwa ajili ya utekelezaji wa kazi kama ilivyoelezwa kwenye Maelezo ya Mahitaji kama ilivyofafanuliwa katika Sehemu ya II

Wazabuni wenye nia ya kufanya kazi ya uwakala ukusanyaji wa mapato yatokanayo na ada za vyoo katika masoko ya Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo. Zabuni hizo ni kama ifuatavyo:-

ZABUNI NAMBA AINA YA ZABUNI
LGA/180/2018 – 2019/ NCS/53 LOT 1 SOKO LA MABIBO
LGA/180/2018 – 2019/ NCS/53 LOT 2 SIMU 2000
LGA/180/2018 – 2019/ NCS/53 LOT 3 SOKO LA SHEKILANGO

Waombaji wanaweza kukagua nyaraka za zabuni na kupata maelezo kutoka kwa Katibu wa Bodi ya Zabuni ya Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo S.L.P. 55068 Dar es Salaam. Ubungo, siku ya Jumatatu hadi ljumaa isipokuwa siku za Sikukuu za Kitaifa kuanzia saa tatu hadi saa tisa na nusu jioni.

Nyaraka za zabuni zinapatikana kwa kuleta barua ya maombi na malipo ya fedha taslimu yasiyorudishwa (Non – refundable) ya shilingi elfu hamsini tu (50,000.00) katika akaunti namba 0150235213900 ya mapato ya ndanl katika Benki ya CRDB ya Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, gharama hizo ni kwa klla “Lot” kwa Mkurugenzi wa Manispaa S.LP. 55068 Ubungo.

Zabuni zote ziwe na nakala halisi (original) moja (1) na nakala kivuli mbili (2) zinazofanana, zilizojazwa kwa usahihi na zilizowekwa kwenye bahasha isiyo na maandishi juu na kuandikwa ‘Zabuni Na. LGA/180/2018 – 2019/NCS/53 LOT No. Ukusanyajl wa mapato yatokanayo na ada za choo, choo cha Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo. Ni lazima kupelekwa kwa Katibu wa Bodi ya Zabuni ya Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo kwa anuani ifuataya-

MKURUGENZL WA HALMASHAURI,
HALMASHAURI YA MANISPAA YA UBUNGO,
S.L.P 55068,
UBUNGO
.

Siku ya mwisho ya kuwasilisha zabuni ni tarehe 24 Aprili, 2019 saa (06.00) sita kamili mchana. Zabuni zitafunguliwa hadharani tarehe 24 Aprili, 2019 saa (06.30) sita na nusu mchana, mbele ya wawakilishi wa wazabuni wanaoamua kuhudhuria katika ufunguaji wa zabuni katika ukumbi wa Manispaa.

Zabuni zitakazochelewa. sehemu ya Zabuni, Zabuni za kielektroniki na Zabuni zisizofunguliwa katika tukio la ufunguaji Zabuni, kwa hali yoyote ile Zabuni hizo hazitakubaliwa kwa tathmini.

BEATRICE R.DOMINIC
MKURUGENZI WA MANISPAA
HALMASHAURI YA MANISPAA YA UBUNGO

WhatsApp
Twitter
Email
LinkedIn
Instagram

Related