eacop-web-logo

MAOMBI YA KUWASILISHA NIA KWA AJILI YA KUSANIFU NA KUTEKELEZA PROGRAMU YA KUFANYA UTAFITI NA KUREJESHA MSITU WA MIKOKO NA ONGEZEKO YAKINIFU LA BIOANUAI YAKE KATIKA BAHARI YA MKOA WA TANGA KATIKA MRADI WA BOMBA LA MAFUTA GHAFI LA AFRIKA MASHARIKI (EACOP) KUMB NA – REQ-00000157

WhatsApp
Twitter
Email
LinkedIn
Instagram

Kampuni ya EACOP inazialika kampuni zenye uzoefu na sifa kuwasilisha maombi ya nia ya kutoa
huduma ya kuandaa, kusimamia na kutekeleza “Kusanifu na Kutekeleza Programu ya Kufanya
Utafiti a Kurejesha Msitu wa Mikoko na ongezeko yakinifu la bioanuai yake katika Bahari ya
Mkoa wa Tanga” katika Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP). Mradi
wa EACOP unahusisha ujenzi na vendeshaji wa bomba litalofukiwa ardhini, linalokatisha mipaka
ya nchi mbili ili kusafirisha mafuta ghafi kutoka eneo la Ziwa Albert nchini Uganda hadi Pwani ya
Mashariki mwa Tanzania kwa ajili ya Kwenda katika Masoko ya Kimataifa. Bomba litaanzia eneo
la Kabaale Wilaya ya Hoima, nchini Uganda, hadi eneo la Chongoleani, Mkoani langa nchini
Tanzania.
MAELEZO MAFUPI YA MAWANDA YA HUDUMA
Kituo cha baharini cha Mradi wa EACOP cha Rasi ya Chongoleani kitakuwa na Sehemu iliyo
nchikavu ya kuhifadhia mafuta, bandari (njia ya ¡uu ya maji) yenye urefu wa kilomita 2
kuelekea ndani ya bahari, na sehemu ya kupakilia mafuta mwisho wa bandari (njia) hiyo. Katika
ujenzi wa njia (bandari) hiyo na matumizi yake sehemu ndogo ya habitati ya
Msitu wa Mikoko itaweza kuathiriwa. Mpango wa Utekelezaji wa Bioanuwai (Biodiversity
Action Plan) umeshaandaliwa na umeonesha kiwango cha awali cha maeneo yatakayowe
za kuathirika. Vifo wa mikoko magondi au mikoko myekundu (Rhizophora mucronate)
vimetokea na kuandikwa mwaka 2021 na
havihusiani kabisa na shughuli za EACOP. Inahitajika Kampuni/Toasisi ya kufanya usanifu na
utekelezaji wa programu ya urejeshaji wa habitati ya msitu wa mikoko; na kutafiti juu ya sababu
zilizopelekea kufa kwa mikoko myekundu katika mdomo wa to Zigi, na matokeo ya utafiti huo
yatumike katika utekelezaj; wa urejeshaji wa mikoko katika Ghuba ya Tanga na kaskazini mwa
Tanzania kwa ujumla ikilenga ongezeko halisi (Net Gains) na ikizingatia vigezo na mbinu bora.
Njia ya kuyafikia hayo inatakiwa we shirikishi ambapo hatua zote zitajumuisha wadau wa ndani na
vikundi vyengine, ikiwa ni pamoja na jumuiya za mitaa, taasisi za serikali na mashirika ya kiraia
Maamuzi ya kutekeleza njia au mbinu zitakazokubaliwayanapaswakuzingatia takwimu za kisayansi
na kuhakikisha ubora wa maamuzi hayo kulingana na hali ya kijamii na mazingira yaliyopo hivi
sasa na mwelekeo wa baadae.

VIGEZO MUHIMU
Kampuni zinazowasilisha nia zinapaswa kutuma maombi pamoja na nyaraka zifuatazo:
 Uthibitisho wa usajili kama shirika/taasisi ambayo shughuli zake zinahusiana na shughuli
za ushirikishaji jamii (kwa mfano urejeshaji wa habitati za baharini unaoshiriki- sha jamii)
 Maelezo mafupi kuhusu uzoefu na uwezo wa kupanga, kusanifu na kutekeleza program za
uendelezaji wa urejeshaji wa misitu ya mikoko, utafiti wa kufa kwa mikoko, kuanzisha
vitalu wya miche ya mikoko, kufanya kazi kwa kushirikiana na kujenga uwezo wa jamii za
pwani, kufanya utafiti, ufuatiliaji na utengenezaji wa ramani za mtandao wa misitu ya
mikoko.
 Mifano ya kazi zinazoonyesha uzoefu wa kufanya kazi zinazofanana na hizo zilizofa- nywa
kipindi cha karibuni, ndani miaka mitano iliyopitaleseni ya biashara.
 Wasifu wa watendaji watakaohusika katika Mradi ikiwa ni Pamoja no nakala za vyeti vyao,
kiwango cha elimu, uzoefu na uwezo wa kutoa huduma inayohitajika.
 Leseni inayofaa kutoka kwa mamlaka husika yo ndani ya nchi kwa ajili ya utoaji wa
huduma hii a Uthibitisho wa Usajili toka Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA) na Cheti
cha Uthibitisho wa Malipo ya Kodi cha mwaka wa hivi karibuni.
 Usajili katika Kanzi Data ya Watoa Huduma wa Ndani ya EWURA (LSSP) au ushahidi
thabiti wa maombi ya usajili wakati wa uwasilishaji wa maombi ya nia hi iliyotan- gazwa.
 Kufuata/kukubaliana na kanuni Za Wazawa za Mambo ya Petroli za Tanzania.
 Uwezo Wa kifedha wa kutoa huduma zinazohitajika ikiwa ni Pamoja na kuwakili- sha
hesabu za fedha za miaka mitatu iliyopita.
 Uthibitisho kutoka mfumo wa usimamizi wa QHSE, taasisi na mchakato kulingana na
viwango wya ndani no wya ki-sekta vinayotu- mika kwa kazi hii. Uthibitisho wa
kukubaliana na sera za Haki za Binadamu, na kupinga rushwa na ufisadi.
Kampuni zenye nia uwezo na rasilimali ya kutoa huduma zilizotajwa hapo juu zinatakiwa kutuma
maombi ya nia yaliyoandaliwa kwa lugha ya Kingereza pamoja na nyaraka zilizobainishwa hapo
juu kupitia barua pepe: [email protected] (ukubwa
usiozidi MB20) kabla au si zaidi ya saa 11:00 jioni Majira ya Afrika Mashariki, tarehe 2nd March2023

Kichwa cha cha barua pepe kiwe: [REQ-00000157] “‘Kusanifu na Kutekeleza Programu ya
Kufanya Utafiti na Kurejesha Msitu wa Mikoko na ongezeko yakinifu la bioanuai yake katika
Bahari ya Mkoa wa Tanga katika Mradi wa EACOP. Maombi yote ya kuonesha nia yawe kati ya
kurasa 10 hadi 20. Maombi yote lazima yawasilishwe kwa lugha ya Kiingereza. Muhimu: EACOP itapitia na kuchambua nyaraka zizotumwa na makampuni yalioone- sha nia kulingana na EOI hii, na kisha kufanya tathmini kulighana na vigezo wya ndani wya EACOP ili kubaini makampuni yenye sifa yatakayojumuishwa kwenye orodha yo awali ya makampuni yenye vigezo. Mwaliko kwa Makampuni kutuma maombi ya zabuni utatumwa kwa Makampuni ya awali yenye vigezo baada ya makampuni hayo kusaini Makubaliano ya Utunzaji wa Taarifa (NDA). Kampuni ya EACOP LTD ina haki ya kuteua au kukataa kampuni na kubaki na maamuzi yake bila kutoa sababu kwa kampuni husika.

WhatsApp
Twitter
Email
LinkedIn
Instagram

Related