UTUMISHI LOGO

TAARIFA KWA UMMA:BEI ELEKEZI YA MBOLEA KWA MSIMU WA KILIMO 2023/2024 (Toleo la 22)

WhatsApp
Twitter
Email
LinkedIn
Instagram

1.0 UTANGULIZI

Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (Tanzania Fertilizer Regulatory Authority – TFRA) kwa niaba ya Wizara ya Kilimo ina jukumu la kutoa bei elekezi ya mbolea kwa wafanyabiashara wa mbolea nchini ambapo mbolea zinatakiwa kuuzwa kwa bei elekezi au chini yake. Hii ni kwa mujibu wa kifungu cha 4(1Xu) cha Sheria ya Mbolea ya Mwaka 2009 na Kanuni ya 56 ya Kanuni za Mbolea za mwaka 2011 kama zilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2017.

Katika kutekelezajukumu lake la kisheria, TFRA imefanya mapitio ya bei elekezi kwa mbolea aina Lisa (9); tano (5) zinazoingizwa kutoka nje (DAP, UREA, CAN, SA na NPKs) na nne (4) zinazozalishwa na viwanda vya mbolea vya Itracom (Fomi Otesha na Fomi Kuzia) na Minjingu (Nafaka Plus na Top Dressing).

Bei hizi zitaanza kutumika kuanzia tarehe 01 Julai, 2023 hadi tarehe 15 Agosti, 2023 (Bei zinapatikana kwenye tovuti ya Wizara ya Kilimo; www.kilimo.go.tz, Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA); www.tfra.go.tz na Of isi za Makatibu Tawala wa Mikoa yote Tanzania Bara). Lengo la kufanya hivyo ni kuhakikisha kuwa mbolea inauzwa kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu zinazosimamia tasnia ya mbolea.

2.0 MJENGEKO WA BEI ELEKEZI

Kwa kuwa mbolea za DAP, UREA, CAN, SA, NPK YARA Cereal na YARA Otesha ni mbolea zinazoingizwa kutoka nje ya nchi, bei elekezi imezingatia gharama za manunuzi, usafirishaji, uingizaji, ufungashaji, usambazaji pamoja na faida ya mfanyabiashara. Aidha kwa mbolea zinazozalishwa nchini (Fomi Otesha, Fomi Kuzia, Fomi Nenepesha, Nafaka Plus, Top Dressing) bei elekezi imezingatia gharama za upatikanaji wa malighafi, uzalishaji, vifungashio, kufungasha, usimamizi na faida ya mzalishaji na muuzaji wa rejareja kusambaza hadi kumfikia mkulima.

3.0 BEI ZA MBOLEA YA RUZUKU KWA WAKULIMA Serikali imeelekeza aina moja ya mbolea kuuzwa kwa bei inayofanana kwa wakulima nchini kote (pan territorial pricing).  Aidha, hakuna mfanyabiashara atakeyeruhusiwa kuuza mbolea nje ya mpango wa ruzuku. Hivyo, tofauti kati ya bei elekezi kwa kila eneo na bei ya mkulima italipwa na Serikali kama ruzuku kwa mkulima kwa lengo la kumpunguzia makali ya bei. Aidha, vifungashio vya ujazo wa kilo tano (5) vitauzwa kwa bei elekezi ya soko.

4.0 USIMAMIZI WA BEI ELEKEZI

Kwa kuwa mbolea zote zinauzwa katika mpango wa ruzuku, Serikali kupitia TFRA imesajili waingizaji na wazalishaji wa mbolea pamoja na mawakala wanaosambaza na kuuza mbolea kwa wakulima na kuwapa namba maalumu za utambulisho. Hata hivyo, ili azma ya Serikali itimie ni muhimu kwa Mamlaka zote husika katika ngazi za Mkoa, Wilaya na Halmashauri

kuhakikisha kuwa kila duka Is pembejeo linabandika namba ya uwakala na bei elekezi sehemu zinazoonekana kwa urahisi kwa wanunuzi. Pia ni vema Mamlaka hizo zikasimamia kwa karibu utekelezaji wa mpango wa ruzuku ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa kuhusu uzingatiaji wa bei za mbolea ya ruzuku na upatikanaji wa mbolea kwa wakulima katika maeneo husika. Aidha, endapo bei hizi hazitaakisi uhalisia wa kijiografia na miundombinu ya eneo husika, nitoe rai kwa Kamati za Pembejeo za Mikoa na Wilaya kupitia na kufanya maboresho kadiri watakavyoona inafaa.

5.0 UDHIBITI WA UTOROSHWAJI WA MBOLEA NJE YA NCHI

Pamoja na kwamba mpango wa ruzuku ya mbolea unalenga kuwapunguzia makali ya bei wakulima; wafanyabiashara wachache wasio waaminifu wanaweza kutumia fursa hiyo kuwalaghai wakulima na kununua mbolea kwa majina yao na baada ya hapo kuitorosha mbolea hiyo kwenda nchi jirani. Halt hii itahatarisha utoshelevu wa mbolea kwa wakulima wetu na pia kuingizia hasara Serikali katika fedha inazotoa kama ruzuku kwa lengo la kumnufaisha mkulima na kuongeza uzalishaji nchini. Pamoja na uelimishaji ambao Serikali inaendelea kuufanya ni vyema Mamlaka zote za Serikali zikashirikiana na wadau wote hususan katika mikoa ya mipakani kama Songwe, Rukwa, Katavi, Kigoma, Kagera, Kilimanjaro, Arusha na mikoa mingine kuhakikisha mbolea ya ruzuku haitoroshwi kwenda nchi jirani.

Vilevile, natoa onyo kali kwa wafanyabiashara wachache wenye tabia hizo au mpango wa kutorosha mbolea ya ruzuku kwenda nchi jirani kutothubutu kufanya hivyo kwani hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao pindi itakapothibitika. Aidha, endapo kutakuwa na haja ya wafanyabiashara kuuza mbolea nje ya nchi, basi wafanye hivyo kwa kuzingatia taratibu na sheria za nchi na sio kutorosha mbolea ya ruzuku.

6.0 HITIMISHO

Ni matumaini ya Serikali kuwa, mpango wa ruzuku ya mbolea utawezesha wakulima kutumia mbolea zaidi na hivyo kuongeza uzalishaji na tija kwa ajili ya utoshelevu wa chakula na kuzalisha malighafi ili kuimarisha uchumi wa viwanda. Hivyo, niwakumbushe wataalamu na wadau wa kilimo kuendelea kutoa ushirikiano wa dhati katika kuwaelimisha wakulima juu ya matumizi sahihi ya mbolea na pembejeo nyingine za kilimo pamoja na kuzingatia kanuni bora za kilimo. Aidha, natoa wito kwa Mamlaka zote katika ngazi za Mikoa, Wilaya na Halmashauri kutoa ushirikiano katika usimamizi wa mbolea ya ruzuku iii Serikali ifikie azma yake na pia mkulima aweze kutumia fursa hii kubadilisha maisha yake kupitia kilimo.

Dkt. Stephan E. Ngailo
MKURUGENZI MTENDAJI
Julai 01, 2023

WhatsApp
Twitter
Email
LinkedIn
Instagram

Related